habari
za kazi na poleni na majukumu, ningependa kushirikiana nanyi nduku
zangu kuufikisha ujumbe huu kwa Watanzania wenzangu ili wapate kujua
kila kinachoendelea na si kupotoshwa na kukubali kutumika.
mimi
ninaitwa Habibu Mchange, ni mfuatiliaji na mchambuzi wa maswala ya
kisiasa, Nimewahi kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
kupitia CHADEMA jimbo la kibaha mjini. Ni mwanachama mtiifu wa CHADEMA
niliyetangazwa kuvuliwa uanachama wa BAVICHA. naomba kuwasilisha.
UNAFIKI WA MBOWE NA VIBARAKA WAKE KWA
WATANZANIA.
Juzi niliandika kuhusu unafiki wa
MBOWE kuwahadaa Watanzania ya kwamba yeye hanunuliki, nilitoa ushuhuda wa MBOWE
kupokea million 100 kutoka kwa ROSTAM AZIZ aliyekuwa mwanamkakati muhimu wa
ushindi wa Urais kwa mgombea wa CCM mwaka 2005 Mheshimiwa JAKAYA KIKWETE,
ambapo pesa hizo zilipokelewa mwezi oktoba 2005 na kumfikia mbowe kupitia kwa
mke wake ndugu LILIAN MTEI MBOWE, na kumfikia MBOWE ambaye kipindi hicho
alikuwa anagombea URAIS kupitia CHADEMA,
hapa mbowe sio tu kwamba alinunuliwa,
alihongwa ama kutumiwa kuwadhoofisha wapinzani waliokuwa na nguvu kipindi
hicho, bali pia alidhihirisha namna gani yeye ni mpinzani mtiifu kwa CCM
(alikubali kutumika) na ni MNAFIKI ALIYETUKUKA.
Leo tarehe 18.12.2013, Magazeti
kadhaa yameripoti juu ya muendelezo wa unafiki wa MBOWE na vibaraka wake.
Magazeti yameandika pamoja na mambo
mengine, kwa ufupi kabisa hivi ifuatavyo.
·
Amemshinikiza
mbunge wa viti maalum ndugu JOYCE MUKYA kukatisha ziara ya kikazi za kibunge alipopangiwa na kumlazimisha wakakutane
nyumbani kwake DUBAI, inawezekana ni kwenda kumlea motto wao FREELADY MBOWE,
ama vinginevyo, lakini huu ni uthibitisho wa UNAFIKI wa MBOWE mbele ya
WATANZANIA, kushiriki kutumia kodi za watanzania kwa matumizi binafsi tena ya
KIMAPENZI na mwanamke aliyemteua kuwa mbunge bila ya kuwa na uwezo wa kukidhi
vigezo vya uteuzi wa UBUNGE ndani ya chama. Kwa sasa JOYCE MUKYA ni mbunge,
Hawara na mama wa motto mmoja aitwaye FREELADY MBOWE, Aliyejifungulia NEW YORK
NCHINI MAREKANI kwa kutumia kodi za Watanzania.
·
MFUASI
WAKE ASIYEJIELEWA – JOSHUA NASSARY, wiki chache zilizopita mbunge huyu wa UPEPO
WA CHAMA alishiriki kumtuhumu ndugu Zitto Kabwe Kuwa anasafiri nchi nyingi ili
apate posho za safari, afadhali aliyemtuhumu kuwa anasafiri, lakini yeye
ameumbuliwa kuwa AMESHIRIKI KUCHUKUA pesa za UMMA WA WATANZANIA, kisha
kutokwenda kushiriki ziara ya kimafunzo kwa maslahi ya nchi. Million 8
alizopewa nassary si pesa nyingi kusema anaweza kutia hasara sana, lakini ni
pesa zinazoweka rehani ule upambanaji anaojitambulisha nao mbele ya jamii, ni
pesa zinazoweka hatiani uwajibikaji anaojitamba nao, ni pesa zinazomdhihirisha
kwamba yeye ni mwizi wa mali ya umma kama walivyo wezi wengine.
UNAFIKI WA
AWALI WA MBOWE NA WAFUASI WAKE.
·
Walijitangaza
hadharani kuwa Hawapokei na wanapinga posho, LAKINI MPAKA SASA WANARAMBA POSHO
KAMA KAWAIDA, na pindi inapotokea imecheleweshwa kulipwa wanasimama kidete
kuidai, mwanachadema pekee asiyepokea posho ni ZITTO KABWE.
·
MBOWE,
kwa mbwe mbwe kubwa alilirudisha gari la kiongozi wa upinzani, kwa nderemo,
vigeregere, matarumbeta waandishi wa habari na vifijo, kuwa kutumia gari la KUB
ni kuwakosea Watanzania, kuwadharirisha na kuzitumia vibaya rasilimali za Taifa
letu, hapa mbowe akajidai ni mzalendo,
tuliokuwa tunamfahamu tulicheka tukamuacha kama ataweza kuhimili alichokisema.
·
MBOWE,
kwa aibu kubwa, akajirudishia gari la KIONGOZI WA UPINZANI, hapa akatafuna
matapishi yake mwenyewe, ila safari hii alifanya kimya kimya.
·
Kwa
masikitiko makubwa hivi sasa mbowe anashirikiana na watuhumiwa wengine
wanaomiliki mali nyingi nje ya nchi ikiwemo uswiz na kwengineko.
·
Mbowe
anamiliki NYUMBA TATU, Pesa na mali nyinginezo nje ya nchi, anamiliki NYUMBA –
AFRIKA YA KUSINI , DUBAI NA MAREKANI. Ameshaitwa kuhojiwa namna alivyoweza
kuzipata NYUMBA HIZO ama kama kuna biashara anafanya zaidi ya UMILIKI WA
DANGURO LA BILLCANAS.
·
Mbowe
anawatetea watoto wa kimasikini wa Kitanzania, ili hali watoto wake wote sio
Watanzania kwa Kuzaliwa, Mpaka sasa anajitamba kwenye vikao vya chama kuwa
motto wake mmoja amezaliwa NEW YORK (Huyu ni mmarekani wa kuzaliwa), Mtoto wake
Mwingine amezaliwa LONDONI huyu ni Muingereza kwa kuzaliwa , na motto wake wa
sasa hivi aliyemzaa na JOYCE MUKYA amezaliwa NEW YORK (Huyu naye pia ni
mmarekani wa kuzaliwa). Uzalendo wa MBOWE uko wapi mpaka sasa?.
UNAFIKI
ZAIDI
Naomba nishirikiane nanyi kujiuliza
maswali machache, UKO WAPI UZALENDO WA MBOWE?,
Kuna Tofauti gani kati ya mali za
Mbowe nje ya Nchi na Vijisenti vya Andrew Chenge?. Mbona hawa wote ni wamiliki
wa mabilioni nje ya nchi?.
Uzalendo wa Mbowe unatokana na nini
kwa Watanzania, kwanini Watanzania Tumpende Mbowe ambaye hatupendi?, hapendi
shule zetu, Hapendi Hospitali zetu, hapendi ardhi yetu ndio maana anamiliki
majumba nchi za nje.
Kwanini tusiamini mbowe anashiriki
kutuchafua kama Taifa hasa vijana akijua kabisa watoto wake yeye sio
Watanzania. Ina maana mbowe hapendi watoto zake waje kuwa viongozi wa Taifa
hili kama ilivyo kwake?, kama la, kwanini amewanyang’anya haki ya wao kuwa
watanzania wa kuzaliwa?.
Nimeamua kujitoa Muhanga kuwaelewesha
masikini wenzangu, walalahoi wenzangu na wanyonge wenzangu, Mbowe sio mtetezi
wetu, mbowe ni mfanyabiashara ambaye mtaji wake ni umasikini wetu, anatutumia
sisi masikini na walalahoi kama mtaji wake wa kisiasa, anatutumia bila ya sisi
kujijua, mbowe ni Tapeli wa kisiasa.
HISTORIA INAMPINGA
Mimi ni mkuumini wa Historia ya
ukombozi, ninafahamu dunia nzima namna nchi zilizohitaji ukombozi namna
zilivyopata ukombozi na namna ya viongozi wao waliowakomboa walivyojitokeza
kwenye jamii.
Mbowe ndio mfanyabiashara pekee
anayejiita mtetezi wa masikini duniani, tangu nimewahi kuifahamu historia ya
ukombozi,
Hakujawahi kutokea Duniani labda
ahera, Masikini wakatetewa na Tajiri, Haijawahi na Jaitawahi kutokea Mfanya
biashara yoyote akapanga kupata hasarfa eti kwa maslahi ya Umma, wafanya
biashara wote wanawaza faida, hata mbowe anawaza faida na sasa anatafuta faida
kwa gharama yoyote.
Tunamsifia Mandela leo, Mandela
hakuwa mfanyabiashara, Mandela hakuwa tajiri, Mandela alichangiwa na masikini
wenzake kuikomboa Arika ya Kusini, Mandela hakuwahi Kuikopesha ANC pesa ili
iwaondoe Makaburuu, Mandela alifanana na jamii aliyotaka kuikomboa na Mandela
alifanikiwa kuikomboa.
Wote tunamsifia Nyerere Hapa
Tanzania, Nyerere Hakuwa Mfanyabiashara, mwalimu Hakuwa Tajiri, mwalimu
Hakuwahi kuikopesha TANU ili kumuondoa MKOLONI, nyerere alichangiwa na masikini
wenzake, aliombewa na walalhoi wenzake na alilindwa na mafukara wenzake.
Mkifano ni mingi, hivyo hivyo kwa
Samora Machel, Kwame Nkuruma, Milton Obote, Robert Mugabe, Kamuzu Banda, Dkt
Martin Lutherking, Mahatma Gandh, Mao Zedong, AmilicaCabra na wengineo wote,
KAMWE KUNGURU WASIOFANANA HAWAWEZI KURUKA PAMOJA.
Nitaendelea kuwafundisha mengi
ninayoyajua kuhusu MBOWE NA CHADEMA kwa kadri itakavyowezekana.
Itoshe tu kusema kwa sasa kwamba
Taifa letu kweli linahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala, linahitaji
mabadiliko makubwa sana ya kisera kimfumo na kimuundo, na ni kweli kabisa CCM
imeshindwa kuendana na Kasi hii ya uhitaji wa mabadiliko, lakini Bahati mbaya
sana watu sahihi wa kufanya Mabadiliko bado hawaonekani, bado Hawapo, Bado
wanafanyabiashara ya kisiasa.
TAHADHARI.
Nimekuwa nikipokea meseji za vitisho
kupitia simu, email na facebook, kuwa nitauawa kama wangwe, ninasema hivi, nipo
tayari kwa yote na mwenye uhakika wa kufanya hivyo asipate shida, anipigie simu
kwa namba yangu 0762178678 NITAMGUATA ALIPO ATIMIZE LENGO LAKE.
Kwangu Daima NYEUPE NI NYEUPE na
NJANO NI NJANO.
Mimi
Habibu Mchange
0762178678
mchangehabibu@yahoo.com
No comments:
Post a Comment