Tuesday, December 17, 2013

MANISPAA YA BUKOBA YAENDELEA KUWAKA MOTO

Hii inafuatia hatua ya baadhi ya madiwani wanaoongozwa na waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki wanaotaka kumg'oa madarakani mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba, Anatory Amani ya kuandika barua ya kutokuwa na imani ya ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambayo iliwasilishwa kwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa hiyo.

Kwa mujibu taarifa madiwani hao wanadai kuwa mkaguzi huyo wa hesabu za serikali anachelesha kusoma taarifa ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili kwa lewngo la kumlinda, madiwani hao chini ya mwavuli wa Balozi Kagasheki wameishaunda mikakati ya mikali ya kumg'oa Meya huyo hata kama mapungufu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake hazitabainika.

No comments:

Post a Comment