TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI
Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa
kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa
SINGIDA na ni mtu wa 300 kitaifa
kujiunga na Chama hiki. Nimejiunga mwaka 1992 siku ya mkutano mkuu kwanza wa
uzinduzi chama uliofanyika mnazi mmoja.
Nimekuwa nikijitolea vya kutosha nguvu,
muda na akili zangu nyingi kukijenga na kukilinda chama hiki mpaka sasa mkoa
wetu wa singida umepata wabunge watatu mmoja wa kuchaguliwa na wawili wa viti
maalum.
Tangu mwaka 1992 mpaka 2011, chadema
imekuwa ikitumia nyumba yangu kama ofisi, nimekuwa nikifanya hivyo kama
kielelezo change cha kudai na kupigania demokrasia ya kweli ndani ya nchi kwa
kuijenga CHADEMA imara.
Kwa kipindi chote hicho nimekubali
kujibana na kuipunja familia yangu stahili zake ili chama chetu kikue kwa kasi
mkoani kwetu, nashukuru mungu wanasingida waliitikia ombi nletu na kutufuta
majozi yaliyotokana na jasho langu kwa kutupatia mbunge mwaka 2010.
Hivyo nimehudhunika sana kwa kitendo
kilichofanywa na wajumbe wa kamati kuu cha kukiuka utaratibu na kujivalisha
mamlaka yasiyowahusu.
HISTORIA YA USALITI KWENYE CHADEMA
Viongozi wa chama chetu wamekuwa na
historian a tabia ya kutubadilishia wasaliti na kuwapachika kila aina ya
shutuma kila kunapokaribia uchaguzi ndani ya chama.
Tuliambiwa na kuaminishwa kuwa KABURU ni
msaliti mkubwa ndani ya chama.
Tukaambiwa na kuaminishwa kuwa CHACHA WANGWE alikuwa msaliti,
tukafanyishwa vikao vya ndani, tukaanzishiwa mikakati mbali mbali kuwa wangwe
ni msaliti na kwamba anatumika.
WANGWE alipofariki hali ikatulia kidogo,
tukaanza kuimba na kumsifia kwamba ni kamanda, tukamuita majina yote ya
kishujaa lakini haikuwa na faida yoyote.
Sasa hivi tumeanza kuaminishwa wasaliti
wengine wapya, safari hii wasaliti hawa wamevuka usaliti na kuwa WAHAINI,
masikitiko yangu ni hawa wahaini ndio wale wale wengine waliokuwa wakikitetea
chama kipindi kinapingwa na waliokuwa wasaliti.
Bahati mbaya sana na cha kufurahisha
kama si cha kusikitisha hakujawahi kutokea Msaliti, Mhaini Wala kiongozi yeyote
anayetuhumiwa kukihujumu chama mwenye asili ya KILIMANJARO ama KASKAZINI kwa
ujumla, wahaini na wasaliti wote wanatokea mikoa yetu sisi wanyonge.
WAVAMIZI NDANI YA CHAMA
Bahati mbaya sana, harakati hizi za
kuibua na kuwashuhulikia hawa wanaoitwa wasaliti zinafanywa na wavamizi ama
wahamiaji ndani ya chama, nitatoa mifano michache muda huu.
1.
GODBLESS
LEMA tulimpokea kwenye chama hiki mwaka 2009 akitokea TLP aliposhindwa
kufanya siasa za ushindani baada ya kushiriki kukiua chama hicho, lema
alikwenda TLP akitokea NCCR-mageuzi aliposhindwa kutimiza malengo yake ya
kisiasa na kushuhudia akikiua chama hicho. Leo LEMA ndio mpambanaji mkuu dhidi
ya Zitto Kabwe, Dokta Kitila mkumbo na demokrasia ya kweli ndani ya chama
chetu, anaambatana na kijana mwengine anaitwa MAWAZO, huyu wakati sisi
tunapambana na CCM mwaka 2010 kuwanadi wagombea wetu wa ubunge urais na
udiwani, yeye alikuwa anagombea udiwani kupitia CCM tuliyokuwa tunaipinga,
ameingia chadema na sasa wale waliokuwa wanampinga akiwa huko leo anawaita
WASALITI na WAHAINI.
2. MCH. MSIGWA naye huyu ni hivyo hivyo tulimpokea CHADEMA baada ya
kushindwa na kuigombanisha NCCR na baadae TLP. Baada ya kuvimaliza vyama hivyo
sasa wamehamia chadema kutugombanisha na kutuharibia chama chetu kwa makusudi
kabisa.
3. Wengine vinara kwenye mgogoro huu ni Tundu Lissu,
bensoni kigaila, john mrema na wengineo hawa ni vijana tuliowapokea kuja
kujenga chama na sio kukibomoa chama kama wanavyofanya
4. TUNDU LISSU yeye ni kinara sana wa kumshambulia zitto kwenye hili,
lakini ninasikitika kusema kuwa Tangu nimekuwa mwanachadema na Tangu
nimemfahamu Lissu alipohamia CHADEMA hajawahi kufanya mkutano hata mmoja wa
kujenga chama ndani ya mkoa wa SINGIDA ukiondoa jimboni kwake. Tumemuona Zitto
akitoka bungeni na mara nyingine hata kigoma kuja kufanya mikitunano maeneo
mbali mbali hapa singida ikiwemo iramba, singida mjini na kwingineko, na
mtakumbuka zitto amewahi kukamatwa na polisi mkoni singida akikinadi chama,
hakuwa lissu. Sasa leo anapotoka mbele na kujinadi kuwa ana mapenzi mazuri na
chama kushinda zitto kabwe ni upuuzi unaopaswa kukemewa kwa nguvu kubwa sana.
Ninasikitika sana kuona Mwenyekiti Mbowe
na Katibu mkuu Slaa wanawakumbatia hawa, ninashangaa sana kuona viongozi hawa
wanakubali kuwa sehemu ya ubakaji huu mkubwa wa demokrasia.
Ninaamini kabisa vijana hawa wanatumiwa
na mwenyekiti na katibu mkuu kuutumia uzoefu wao walioutumia kwenye vyama vyao
vya awali mpaka kuviua.
KUHUSU
KAMATI KUU NA MAAMUZI YAKE.
Uamuzi wa kuwavua nyadhifa zitto kabwe
na wenzake kwa madai ya kuwa na mkakati wa siri wa uchaguzi, ni uamuzi wa
kipuuzi na wa kupuuzwa, kwenye hili kamati kuu imedhihirisha namna gani
inaundwa na watu wasio na weledi na hawaongozwi na misingi na taratibu za
chama.
Katika chama chochote kile, kamati kuu
haiwezi kuwa mshitaki mkuu, hiyo hiyo iwe mwendesha mashitaka, hiyo hiyo iwe
shahidi, hiyo hiyo iwe hakiku na hiyo hiyo iwe muandika hukumu. Hapa
wamedhihirisha ni namna gani wanaongozwa na Hisia na chuki zinazotawaliwa na
hofu ya uchaguzi ndani ya chama.
Kamati kuu hii ya sasa haipo kwa ajili
ya maslahi ya wanachama na chama kwa ujumla, ipo kwa maslahi ya mbowe na slaa pengine
na watu wa kaskazini.
Kwa hiyo kuwazuia watu wenye mawazo
tofauti na wao na kuwaita wasaliti na wahaini ni sawa kuasisi na kuimiza
mpasuko ndani ya chama, maana kuna mambo kamati kuu inaweza kufanya na kuna
mengine haiwezi, hii haiwezi kufanya hili walilolifanya sasa hawawezi
kulifanya.
Nionavyo mimi na wanachama ninaowaongoza
hapa singida ni kwamba kamati kuu imekurupuka na kufanya maamuzi yaliyotawaliwa
na hofu, chuki na uroho wa madaraka dhidi ya zitto kabwe na wenzake
walioonyesha nia thabiti ya kukivusha chama kwenye harakati za kuilikomboa
Taifa.
MSIMAMO WA CHAMA
SINGIDA
(i)
Tunalaani, kuipinga na kuikemea kamati kuu ya chama
dhidi ya maamuzi yao haya ya kipuuzi yaliyojaa chuki, hofu na wasiwasi mwingi
kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ya chama
(ii)
Tunamtaka mwenyekiti na katibu mkuu waitishe mara moja
mkutano wa baraza kuu la chama kutolea maamuzi suala hilo.
(iii)
Tunamtaka katibu mkuu awazuie wakurugenzi na maafisa
wake aliowatuma kusambaa mikoani kusambaza waraka wa siri unaowachafua zitto na
kitila na kwamba kufanya hivyo ni kujidharirisha wao wenyewe.
(iv)
Tunampa onyo kali katibu mkuu Dkt. Slaa kuwa
asithubutu kukanyaga SINGIDA ikiwa bado hajayafanyia kazi maelekezo yetiu hapo
juu, kuzunguka kwake mikoani baada ya kumvua vyeo zitto ni kwenda kuthibitisha
kuwa amefanya makusudi mpango wake huo.
(v)
Tunapenda wanachadema na watanzania watambue kuwa
Hatuna Imani na Mwenyekiti wa Taifa wa chama, Katibu Mkuu wa Chama, Kamati kuu
kwa ujumla na tunamuagiza mbowe aivunje mara moja kisha nay eye ajiudhuru.
MWISHO
Kutokutii
maamizio yetu haya ni kusababisha mgogoro usiokuwa na kikomo ndani ya chama
hiki,
Singida
tunasema kuwa ‘’ kamati kuu inaweza kumvua zitto kabwe uongozi, inaweza
kumuondolea heshima yake ndani ya jamii, inaweza pia kumsingizia kila aina ya
uwongo itakavyo, lakini kamwe kamati kuu haiwezi KUZUIA MPASUKO NDANI YA
CHADEMA.’’
Kwa kuzingatia utangulizi wangu hapo
mwanzo, na kwa kuona ukweli kwamba chama chetu sasa kimevamiwa na kuwa na vyama
viwili ndani ya chama kimoja,
Nimeonelea ni vyema sasa niilinde na
kuithibitisha dhamira yangu ya demokrasia ya kweli, nimeona ni vema nihakikishe
demokrasia tunayoiimba tunaitenda kwa vitendo.
Kwa misingi hiyo sasa, nimeamua kukaa
pembeni ya udhalimu huu wa demokrasia unaoasisiwa na viongozi wakuu wa chama
wanaoogopa kivuli cha uchaguzi mkuu wa ndani ya chama,
Nimeona ni vema sasa niuthibitishie umma
wa Tanzania kuwa kwenye chadema unaruhusiwa kugombea vyeo na nafasi zote
isipokuwa uenyekiti wa Taifa ndio maana zitto tuliyemuunga mkono leo hii
anashambuliwa kwa dhamira yake safi ya kidemokrasia.
Nimechoka sasa, nimebadili mawazo, sipo
tayari tena kuwa msukule wa fikra mbele ya watu wanaopenda kuigiza na kujifanya
watetezi wa wanyonge kumbe ni wanafiki wa kutupwa.
Nimememuandikia barua katibu wangu wa
mkoa kumueleza maamuzi yangu ya kujiudhuru uenyekiti wa mkoa, sihitaji tena
kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho hakitendi kinachoyasema, sihitaji
tena kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho dakika na saa yoyote unaweza ukageuzwa
na ukaitwa msaliti na muhaini wa aina ya kopekee.
Mimi kitundu, sihitaji kuendelea kuwa
dalali wa mafanikio ya kisiasa kwa ajili ya watu wa kaskazini dhidi ya
watanzania wenzangu.
Nimejiuzuru uenyekiti wa mkoa wa SINGIDA
kuanzia leo tarehe 3.11.2013 na kuahidi kuwa nitapambana mpaka mwisho wa tone
la damu ya uhai wangu kuhakikisha demokrasia ya ndani ya chama hiki
inaheshimiwa na kwamba watanzania hawadanganywi tena.
Nawashukuru sana.
Wilfred Noel Kitundu
Mwenyekiti Mkoa SINGIDA
Muasisi na mlezi wa CHADEMA Singida
1992-2013
Mjumbe wa Baraza Kuu TAIFA 1992 – 2013
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa 1992-2013
+255786215181/0764619335
WILFRED
NOEL KITUNDU
MWENYEKITI
CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
KATIBU
WA CHADEMA MKOA
S.L.P
260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda kukuarifu kuwa nimeamua
kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa
kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai demokrasia ya kweli
ndani ya chama.
Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa
kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mwanachama wa 300 kitaifa,
hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa
sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia uliopitiliza
Maamuzi na vitendo vinavyoendelea ndani
ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na udharirishaji wa demokrasia ya kweli
tunayoihubiri mbele ya umma.
Kwa barua hii basi, nimeonelea bora
upate ufahamu huo kuwa si vema mimi kuendelea kupingana na dhamira yangu
inayonituma kuwa mwanademokrasia wa kweli.
Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza
mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani yenu
tayari.
Ninatanguliza shukrani zangu za dhati
kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywa na kamati kuu ya chama.
Kusimamia haki, katiba na misingi ya
chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna yoyote ile sitaweza kuwa tayari kufumba
macho pindi ujinga wa namna hii unapoendelea kutekelezwa kwa uwoga wa uchaguzi.
Nakutakia kila la heri kwenye majukumu
yako.
………………………………………………….
Wilfred N. Kitundu
0764619335/0786215181
No comments:
Post a Comment