Saturday, December 22, 2012

MKUTANO MKUU WA SABA WA BURUTE SACCOS MKOANI KAGERA

 Wajumbe wa sekretatieti ya BURUTE ambacho ni chama cha akiba na mikopo kinachoundwa na walimu wa halmashauri za wilaya ya Misenyi na Bukoba.
 Meneja wa BURUTE, Abbas Kabakama akitoa maelekezo kwa wajumbe wa mkutano mkuu.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa BURUTE.
 Mwenyekiti wa BURUTE, Regina Mulokozi akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa kawaida wa BURUTE, ulifanyika kwenye ukumbi wa chama cha msalaba mwekundu ulioko katika manispaa ya Bukoba.
 Mwenyekiti wa chama cha walimu (CWT) mkoa wa Kagera, Dauda Bilikesi akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa BURUTE wa mwaka 2012, aliwahimiza walimu wakope mikopo kwa busara, watumie vizuri mikopo wanayoipata hasa kwa kuanzisha shughuli za kuwaongeza kipato, aliwaonya wajiepushe na taasisi za kitapeli zinazowakopesha fedha hasa kwa kuwatoza riba kubwa.
Mwakilishi wa kampuni ya uhasibu wa CIBE, Simon Paul, kampuni ya CIBE ndio inafanya kazi ya ukaguzi wa nje wa BURUTE, kulia ni afisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi.

No comments:

Post a Comment