Wednesday, December 19, 2012

UZINDUZI WA ALBAM YA YESU NI MWEMA KAGERA

CHRISTINA SHUSHO KUWASHA MOTO BUKOBA JUMAPILI 23/12/12

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Christina Shusho atakuwa miongoni mwa waimbaji wa kimataifa watakaopamba uzinduzi wa album album ya “Yesu ni mwema” iliyoimbwa na kundi la KAPOTIVE Star Singers-Bukoba lenye makao yake makuu manispaa ya Bukoba.

Uzinduzi wa album ya album ya KAPOTIVE utafanyika tar. 23/12/12 katika ukumbi wa LINAS CLUB kuanzia saa 8 mchana hadi 1 jioni.  Pamoja na Christina Shusho, pia atakuwepo mwimbaji ambae ndie mwimbaji bora wa nyimbo za Injili nchini Uganda Padre Anthony Musaala, kwaya ya Mt. Josephina Bakhita ya Rwamishenye, kwaya ya vijana ya KKKT ya Bukoba mjini, na kwaya ya SDA pia ya Bukoba mjini.

Kiingilio katika uzinduzi huo kitakuwa 15,000 kwa mtu mmoja(Single size ticket), 25,000 kwa watu wawili(double size ticket), 50,000 watu wanne ( family size ticket).

No comments:

Post a Comment