Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera, Philip Kalangi, akimpokea katibu tawala wa mkoa wa Kagera Nassor Mnambila alipowasili kwenye uwanja wa uhuru kuhudhuria maadhimisho ya kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia mkoani Kagera.
Ujumbe uliokuwa ukitolewa na waandamanaji.
JUMLA ya makosa ya ukatili wa kijinsia 612 yalitokea kwenye
maeneo mbalimbali yaliyoko mkoa Kagera
katika kipindi cha kuanzia kipindi cha mwezi Januari hadi mwezi Novemba, mwaka
huu.
Makosa hayo yaliyotokea
yalibainishwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi
(kushoto) kwenye taarifa yake aliyoitoa mbele ya katibu tawala wa mkoa wa Kagera Nassor
Mnambila wakati maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika kwenye
viwanja vya uhuru vilivyoko katika manispaa ya Bukoba.
Kwenye taarifa hiyo Kalangi aliyataja makosa ya ukatili wa
kijinsia kuwa ni pamoja na 306 ya ubakaji, 12 ya kulawiti, 135 ya shambulio na
kipigo, 18 ya kutorosha wanafunzi, 96 ya kutelekeza familia, 20 dhidi ya
ukatili wa watoto na 25 ya mimba kwa wanafunzi.
Alisema katika kipindi hicho kesi za makosa ya ukatili wa kijinsia 170 zilifikishwa mahakamani ,
aliendelea kusema kuwakesi za makosa 56
bado ziko kwenye upelelezi, kesi za makosa 50 zilipata mafanikio na kesi za makosa
80 zilikosa mafanikio.
Kalangi alisema jeshi la polisi mkoani Kagera litahakikisha
linaimarisha amani na utulivu na maendeleo kwa kuchukua hatua mbalimbali dhidi
ya wale wote wanaofanya vitendo viovu kwa kushirikiana na wadau wengine wa
usalama chini ya dawati la jinsia la jeshi la polisi.
Aliendelea kusema kuwa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ni
uharifu kama uharifu mwingine wowote, “jeshi la polisi halitamwonea aibu mtu
yotote atakayejihusisha na masuala ya kutekeleza masuala ya ukatili ya
kijinsia, tutamshughulikia bila kujali cheo chake, rangi yake na nafasi yake
aliyonayo ndani ya jamii” alisema.
Katibu tawala wa mkoa wa Kagera Nassor Mnambila aliyekuwa
mgeni rasmi wakati wa maadhimisho hayo alilipongeza jeshi la polisi mkoani humo
kwa juhudi linalozifanya za kupambana na vitendo vya uharifu mkoani Kagera.
Alilitaka jeshi hilo lisilegeze kamba badala yake
liwashughulikie kikamilifu wale wote wanaijuhusisha na vitendo vunavyohatarisha
amani na utulivu ndani ya jamii, alisema serikali mkoani Kagera itaendelea
kuliunga mkono jeshi hilo ili likamilishe adhima yake ya kuthibiti kabisa
vitendo vya uharifu mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment