UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Rais
Kikwete awasili Dodoma kuhutubia Bunge Maalum la Katiba
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo, Alhamisi, Machi
20, 2014, amewasili mjini Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambako
miongoni mwa mambo mengine atakuwa Mgeni Rasmi na atahutubia Bunge Maalum la
Katiba kesho, Ijumaa, Machi 21, 2014.
Muda mfupi baada ya
kuwa amewasili na kulakiwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda
kwenye Uwanja wa Ndege wa Mjini Dodoma, Rais Kikwete ameendesha Kikao cha
Baraza la Mawaziri lake kwenye Ukumbi wa TAMISEMI ikiwa ni shughuli yake ya
kwanza katika ziara hiyo fupi ya Mkoa wa Dodoma.
Kesho, Ijumaa, Rais
Kikwete atakuwa mgeni rasmi na atahutubia Bunge Maalum la Katiba kutokana na
mwaliko wa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mheshimiwa Samuel J. Sitta ambaye alimwalika Rais Kikwete kwa barua
yake ya Machi 15, mwaka huu, ambayo ilijibiwa Machi 18, mwaka huu, kwa Rais
Kikwete kukubali mwaliko huo.
Mwaliko huo wa
Mheshimiwa Sitta kwa Rais Kikwete umetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 7(1) (g) na
Kanuni 75 (1) ya Kanuni za Bunge Maalum ambazo zinampa Mwenyekiti wa Bunge
Maalum madaraka ya kumwalika Mgeni Rasmi aweze kuhutubia Bunge Maalum.
Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
20 Machi, 2013
No comments:
Post a Comment