Wednesday, March 19, 2014

PAC YAKUTANA NA BOT

Kamati ya PAC Leo imekutana na Benki Kuu ya Tanzania kupokea Maelezo kuhusu fedha tshs 201 bilioni za akaunti ya Tegeta Escrow. Fedha hizi zinahusiana na mkataba IPTL. PAC ina wasiwasi kwamba TANESCO, kwa mujibu wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi zinazofikia zaidi ya tshs 200 bilioni kwa kampuni iliyonunua IPTL.
Kamati imeamua kwamba;

1) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanya ukaguzi maalumu wa suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti maalumu ya tegeta escrow.
2) TAKUKURU waanze uchunguzi wa mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki wa kampuni hiyo na uhamishaji wa umiliki kwenda kampuni ya PAP.

Kamati imeshangazwa na kitendo cha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kuanzisha ukaguzi maalumu wakati yeye mwenyewe ni mtia saini kwenye hati ya kutoa fedha hizo na mshiriki mkubwa katika mchakato mzima. Hivyo, kamati imeagiza ukaguzi maalumu kutoka kamati PAC ili kuweza kupata ukweli.

PAC imetoa mpaka mwisho wa mwezi Aprili kwa taarifa ya ukaguzi huo kuwa umekamilika na kuwataka wahusika wote wa mchakato wa IPTL kusubiri matokeo ya ukaguzi.

PAC imetaka pia maamuzi ya mahakama kuheshimiwa.

Imetolewa na
Mwenyekiti PAC-Zitto Kabwe(MB)
Dodoma
Jumapili 16 Mechi 2014

No comments:

Post a Comment