Idara ya Maendeleo ya Jamii na
Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera imetumia
jumla ya Sh.milioni 48,000,900/= kuhudumia watoto mbalimbali waishio kwenye
mazingira hataraishi kwenye Halmashauri hii katika kipindi cha mwaka miaka
mitatu iliyopita.
Mratibu wa Ukimwi wa Halmashauri
ya Wilaya Missenyi, Rwegerera Katabaro alisema hayo mjini hapa kuwa kiasi hicho
cha fedha kilitumika kuwalipia karo na kuwanunulia vifaa vya kuandikia
wanafunzi 2700 wanaosoma shule
mbalimbali za msingi na sekondari katika Halmashauri hii.
Akizungumzia tatizo la watoto
kuishi katika mazingira hatarishi, Katabaro alisema baadhi yao wanatoka kwenye
familia maskini sana, wachache ni yatima wakati wengine wametelekezwa tu na
wazazi wao; hivyo kulazimika kuishi na bibi zao wasio na uwezo.
Kutokana na hali ngumu ya maisha,
walezi hao huwashawishi watoto hao kujiingiza kwenye shughuli za vibarua kwa
lengo la kuzisaidia familia zao kimaisha.
‘’Baadhi ya watoto hawa ulazimika
kufanya vibarua katika mashamba au kujiajiri kwa kuendesha baiskeli kwa kubeba
abiria maarufu kama Asecdo’’ alisema Katabaro.
Aidha, Katabaro alieleza kuwa
Idara hiyo inakusudia kuimarisha Kamati za kumlinda mtoto katika ngazi mbalimbali
na kuwaagiza watendaji wa kata na vijiji kuwatambua watoto wote waishio kwenye
mazingira hatarishi au mazingira magumuu katika maeneo yao ili waweze
kufuatiliwa.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo,
Halmashauri ya Wilaya ina jumla ya watoto 5036 waishio katika mazingira magumu,
na jumla ya watoto 900 kati yao wanahudumiwa na Halmashauri kwa mwaka, hata
hivyo asasi zisizo za serikali au za kidini nazo zinatoa
mchango mkubwa katika kuwasaidia wanaobaki.
Alisema jamii inawajibu wa
kuangalia namna bora ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
kwani watoto wa leo ni taifa la kesho, kuachana na tamaduni za kusaidia wakati
wa raha
“Jamii ni lazima ibadilike na
kuachana na huu utamaduni wa kuchangia katika sherehe tu bali moyo huo
utumike namna ya kuwasaidia watoto
hawa’’ alisema Katabaro.
Hata hivyo alisema ili kupunguza
athari zitokanazo na janga la UKIMWI
Halmashauri imeandaa mkakati malum kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wa ndani na nje ili ifikapo mwaka 2017 athari zitokanazo na janga la Ukimwi
zipungue hadi asilimia 30.
No comments:
Post a Comment