WAKANDARASI wazalendo hapa nchini wameshuriwa
kuimarisha umoja unaowaunganisha ili waweze kukabiliana na changamoto
zinazowakabili zinazokwamisha katika mchakato wa kushinda zabuni.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya ujenzi ya TEKI mhandisi Emmanuel Bishanga ambaye
pia ni katibu wa umoja wa kandarasi wa mkoa wa Kagera (TASEKA)
wakati akitolea ufafanuzi malalamiko yanatolewa na baadhi
ya wakandarasi wanaodai kuwa zabuni za ujenzi wa barabara zinatolewa kwa
upendeleo hasa kwa makandarasi wenye uwezo mkubwa.
Bishanga amesema umoja wa
wakandarasi unapokuwa hai unaweza kuleta wawekezaji wenye mitambo mikubwa ya
ujenzi ambayo ambayo wakandarasi wenye uwezo mdogo wanaweza kuikodisha
tofauti na utaratibu wa sasa ambao wakandarasi wanaitumia wa kukodi mitambo
toka kwa makandarasi wenye uwezo mkubwa wanaoshindana nao zinapotangazwa zabuni.
Alisema si
kweli kwamba TANROADS inatoa zabuni za ujenzi wa barabara kwa upendeleo hasa
kwa wakandarasi wakubwa, Bishanga alisema wakala hao wa barabara wanatoa zabuni
kwa kuangalia vigezo vingi.
"Ndugu mwandishi kawaida zabuni ufunguliwa
mbele ya wakandarasi wote wanaokuwa wameomba kazi, zikifunguliwa kila ombi moja
moja uchambulisha hapo ndipo mshindi wa zabuni utangazwa" mhandisi huyo.
"Mimi siwatetei maofisa wa TANROADS wanaogawa zabuni ninachokisema kulingana na uzoefu nilionao
kwamba wanaonyimwa zabuni ni makandarasi wasio na sifa ya kutekeleza miradi ya
ujenzi wa barabara, makandarasi wasio na sifa ni wale wasio na mitaji, vitendea
kazi na wsenye sifa za kutokuwa waaminifu hasa katika kukamilisha kazi
wanazopewa" alisema Bishanga.
Naye Manyus Rweyendelela ambaye pia ni
mkandarasi aliwaomba wakandarasi watimize vigezo vyote vinavyotakiwa wakati wa
kuomba zabuni.
"Sio siri taarifa zinazoenezwa za kuichafua
TANROADS zinaenezwa na makandarasi wanakosa tenda kwqa kushindwa kutimiza
vigezo" Alisema.
"Mimi ni mkandarasi mdogo ila huwa ninaomba
kazi TANROADS, wakati mwingine nakosa wakati mwingine napata, nasema tangu
nianze kuomba zabuni TANROADS sijawahi kutoa rushwa ili nishinde zabuni,
wanaoeneza taarifa za upotoshaji wana mawazo mufilisi" alisema Manyus.
Kwa upande wake Julius Basinda alisema ndani ya
TANROADS hakuna namna mkandarasi anaweza kushinda zabuni kwa kutoa rushwa
siku ya kufungua zabuni kila kitu huwekwa hadharani.
"Ninachosema ushindi wa zabuni ni kutimiza
vigezo, ndugu zangu wakandarasi msijidanganye kwa kufikiri kwamba mtashinda
zabuni kwa maneno au kwa kutumia rushwa hali hiyo ilishabadili siku
nyingi" alimaliza.
No comments:
Post a Comment