Barabara ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha
Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu
umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za
Milenia (Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa
barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya
kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika
kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya
na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Saturday, April 13, 2013
RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI BARABARA YA TANGA HADI HOROHOTO
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi barabara ya Tanga –
Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa
kilomita 65.14 akisaidiana na Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu
wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), Balozi wa Marekani
nchini Mhe Alfonso Lenhardt, Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu
ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia
mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia
Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation –
MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya
Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara.
Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua fursa za kibiashara kati
ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la
Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kufungua barabara ya Tanga –
Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa
kilomita 65.14 akiwa ameongiozana na Naibu waziri wa wizara ya ujenzi,
Mhe Gerson Lwenge (kulia), Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa
Mfuko wa Changamoto za Milenia wa Marekani (MCC), Balozi wa Marekani
nchini Mhe Alfonso Lenhardt, na mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Chiku Gallawa
(kushoto)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment