BAADHI ya wadau wa sekta ya elimu
katika mkoa wa Kagera wameishauri serikali kuzifungia kabisa shule zinazobainika
kujihusisha na wizi wa mitihani pamoja na kuwachukulia hatua za kali
baadhi wamiliki wa shule hizo na maofisa wa serikali
wanaoshirikiana nao ili iweze kukuza na kuimarisha sekta hiyo nchini.
Wadau sekta hiyo wametoa ushauri huo
leo kwa nyakati tofauti wakati wakieleza sababu mbalimbali zinazochangia
kudumaza ukuaji wa kiwango cha elimu hapa nchini.
Walisema kushuka kwa kiwango cha
elimu hapa nchini kunachangiwa na tabia ya kuvuja kwa mitihani, walisema
kuvuja kwa mitihani kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya
wamiliki wa shule binafsi ambao hupenda shule zao zionekane maarufu zaidi
ya shule nyingine.
Mwandishi maarufu wa vitabu hapa
nchini vinavyohusiana na masuala ya kilimo Pius Ngeze ambaye pia ni
mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha mapinduzi (CCM) wa mkoa wa Kagera
alisema wamiliki wa shule wanaoshirikiana na baadhi ya maofisa wa baraza la
mitihani kuiba mitihani kwamba wanaua nchi.
Ngeze aliwafananisha ya
wamiliki wa shule wanaowapa majibu wanafunzi ili shule zao zionekane zinafanya
vizuri sawa na wauwaji, alisema mmiliki wa shule anayewampa wanafunzi majibu ya
mtihani ili shule yake ionekana inafanya vizuri kuwa anakuwa anawamchimbia kaburi.
Leonidas Mgashe, ambaye ni
afisa utalii wa kampuni ya utalii ya walkgard iliyoko mkoani Kagera anasema kuna
baadhi ya wamiliki wa shule binafsi wanaotaka shule zao zionekane maarufu
zaidi ya shule nyingine, aliwatuhumu kuwa wamiliki hao ndio wanajihusisha na
vitendo vya wizi wa mitihani ili shule zao zifanye vizuri waweze kupata wateja
wengi zaidi.
Naye, mwenyekiti wa baraza la
usafiri wa majini na nchi kavu mkoani Kagera, Michael Cleophace alitoa ushauri
kwa watendaji wa baraza la mitihani
kuzingatia maadili ya kazi yao ili
wajiepushe na vishawishi waweze kuinua na kuimarisha kiwango cha elimu hapa
nchini.
Alimaliza kwa kuiomba serikali kubuni
mikakati itakayosaidia kuthibiti mianya yote inayochangia kuvuja kwa mitihani
inayotungwa na baraza la mitihani.
No comments:
Post a Comment