MTU mmoja anayetuhumiwa kwa
ujangili ameuwawa baada mapambano makali ya kurushiana risasi kati ya
askari jeshi la polisi mkoani Kagera lililoshirikiana
na askari wa idara ya wanyama pori na kundi la watuhumiwa wa ujangili ndani ya
pori la hifadhi ya taifa la Burigi lililoko wilayani Ngara.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la
polisi mkoani Kagera, Philip Kalangi amesema mapambano hayo yalianza pale majangili
hayo yaliyokuwa na silaha mbalimbali za kivita yalipoanza kujiami kwa kwa
kuwarushia askari risasi ambao walikuwa wakiyaamulu majangili hayo
yajisalimishe.
Katika tukio jingine kamanda Kalangi amewaambia waandishi wa
habari kuwa jeshi la polisi linamshikilia Joshua Mlindwa (25) mhaya mkazi wa
kata kashai mhutumiwa wa kuvunja ofisi ya shule ya sekondari ya Bukoba kwa kutumia funguo bandia kuiba yeti vya taaluma 131.
Akisimulia tukio hilo amesema mtuhumiwa amekamatwa baada ya kuwekewa
mtego, Kalangi amesema kuwa mtuhumiwa
alikuwa akidai uongozi wa shule ya sekondari ya Bukoba impatie shilingi milioni
6 ambayo alitaka ilipwe kwa njia ya M pesa ili aweze kurejesha vyeti hivyo la
sivyo angeviaribu kwa kuvichoma moto.
Kamanda Kalangi akionyesha vyeti ambavyo vilikuwa vimeibiwa na mtuhumiwa anayeshikiliwa na jeshi la polisi n i vyeti vya taaluma vya wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari ya Bukoba iliyoko katika manispaa ya Bukoba.Kamanda akionyesha funguo bandia.
No comments:
Post a Comment