Tuesday, April 30, 2013

MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA KUFANYIKA MKOANI KAGERA

MKOA wa Kagera utakuwa mwenyeji wa  maadhimisho ya kumbukumbu siku   ya mashujaa  itakayoadhimishwa mwezi julai 25, mwaka huu.

Akiongea na waandishi mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu  Fabian Massaw wakati wa kikao kilichokuwa na lengo la kujadili  wajibu wa wadau wa habari katika maandalizi na kushiriki katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa huyo.

Katika kikao hicho Massawe aliwaambia waandishi wa habari  kuwa maadhimisho hayo yatafanyika kwenye maeneo ya kambi ya kijeshi la wananchi (JWTZ)  ya  Kaboya iliyoko wilayani Muleba.

Mkuu huyo wa mkoa aliviomba vyombo vya habari kuwahamasisha wananchi ili washiriki kikamilifu kwenye mchakato mzima wa maandalizi ya maadhimisho hayo.

Alisema maandalizi ya maadhimisho hayo kuwa yanahitaji nguvu ya pamoja ili yaweze kufanikiwa kwa asilimia kubwa, aliendelea kusema kuwa maandalizi ya maadhimisho yanaendelea vizuri.

Katika kufanikisha maandalizi hayo Massawe aliwaomba wananchi wazingatie usafi ili wageni wataofika kushuhudia maadhimisho hayo toka maeneo mbalimbali wakute mji wa Bukoba ukiwa  safi.

Alisema katika maadhimisho hayo mkoa wa Kagera unatarajiaa kupokea wageni zaidi ya wageni 1,500 wakiwemo mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali  pamoja na wageni wengine toka nje ya nchi.

Aliwahimiza  kwa kuwahimiza wananchi wachangamkie fursa  mbalimbali zitakazotokana na maadhimisho ya siku hiyo, “ndugu wa waandishi wageni watakuwa wengi huu ni wakati wa wananchi kuwa wabunifu kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kuwapatia kipato” alimaliza

Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa mwaka yaliadhimishwa mkoani Mtwara.

No comments:

Post a Comment