MKOA wa Kagera utakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya kumbukumbu siku ya
mashujaa itakayoadhimishwa mwezi julai 25,
mwaka huu.
Akiongea na waandishi mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali
mstaafu Fabian Massaw wakati wa kikao
kilichokuwa na lengo la kujadili wajibu
wa wadau wa habari katika maandalizi na kushiriki katika maadhimisho ya siku ya
kumbukumbu ya mashujaa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa huyo.
Katika kikao hicho Massawe aliwaambia waandishi wa habari kuwa maadhimisho hayo yatafanyika kwenye
maeneo ya kambi ya kijeshi la wananchi (JWTZ) ya Kaboya iliyoko wilayani Muleba.
Mkuu huyo wa mkoa aliviomba vyombo vya habari kuwahamasisha
wananchi ili washiriki kikamilifu kwenye mchakato mzima wa maandalizi ya
maadhimisho hayo.
Alisema maandalizi ya maadhimisho hayo kuwa yanahitaji nguvu
ya pamoja ili yaweze kufanikiwa kwa asilimia kubwa, aliendelea kusema kuwa
maandalizi ya maadhimisho yanaendelea vizuri.
Katika kufanikisha maandalizi hayo Massawe aliwaomba
wananchi wazingatie usafi ili wageni wataofika kushuhudia maadhimisho hayo toka
maeneo mbalimbali wakute mji wa Bukoba ukiwa
safi.
Alisema katika maadhimisho hayo mkoa wa Kagera unatarajiaa
kupokea wageni zaidi ya wageni 1,500 wakiwemo mabalozi wanaowakilisha nchi
mbalimbali pamoja na wageni wengine toka
nje ya nchi.
Aliwahimiza kwa kuwahimiza
wananchi wachangamkie fursa mbalimbali
zitakazotokana na maadhimisho ya siku hiyo, “ndugu wa waandishi wageni watakuwa
wengi huu ni wakati wa wananchi kuwa wabunifu kwa kujihusisha na shughuli
mbalimbali za kuwapatia kipato” alimaliza
Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa mwaka
yaliadhimishwa mkoani Mtwara.
Tuesday, April 30, 2013
Sunday, April 28, 2013
MAMBO YA SHEREHE ZA MUUNGANO WA NCHI ZA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR
Ndege za kivita zikifanya maonesho katik sherehe za Miaka 49 ya Muungano jijini Dar es salaam leo.Zenye rangi ya njano zinazomwaga rangi za bendera za Taifa ni ndege za mafunzo na zingine za kijivu
ni za kivita.
Thursday, April 25, 2013
BALOZI Dr. KAMALA NA WASOMI
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye
miwani) akiwa na Wanafunzi kutoka Tanzania wanaosoma masuala ya Maji
katika Taasisi ya Elimu ya Maji ya Kimataifa (UNESCO), Delft Uholanzi.
Watanzania kumi na sita kutoka Tanzania wamehitimu katika fani za
usambazaji wa maji, maji na mazingira, usimamizi wa raslimali za maji na
utatuzi wa migogoro ya maji.
WAZIRI MKUU DODOMA
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Maaskofu kutoka Kanda ya Ziwa
waliotembelea Bunge Aprili 25,2013. kutoka kushoto ni Alex Lwakusumbwa,
Z. Isaya na Charles Sekelwa. Wapili kulia ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel
Maige. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Viti Maalum na Mkuuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 25,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Viti Maalum na Mkuuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 25,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
MATUKIO MBALIMBALI IKULU
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya
mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bw John haule kwa Balozi wa
Bangladesh nchini Mhe Wahidur Rahman baada ya kupokea hati zake za
utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini
Dar es salam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa na Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage kwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Kuwait nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam. Kushoto ni Bw Abdul Rahman Al-Hashim, Meneja wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait aliyeongozana na balozi huyo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa na Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage kwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Kuwait nchini Mhe Yacoub Y. Alsanad kabla ya ya kupokea hati zake za utambulisho na kisha kufanya naye mazungumzo leo April 25, Ikulu jijini Dar es salam. Kushoto ni Bw Abdul Rahman Al-Hashim, Meneja wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait aliyeongozana na balozi huyo.
Wednesday, April 24, 2013
WAKANDARASI WAZALENDO WAPEWA USHAURI
WAKANDARASI wazalendo hapa nchini wameshuriwa
kuimarisha umoja unaowaunganisha ili waweze kukabiliana na changamoto
zinazowakabili zinazokwamisha katika mchakato wa kushinda zabuni.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya ujenzi ya TEKI mhandisi Emmanuel Bishanga ambaye
pia ni katibu wa umoja wa kandarasi wa mkoa wa Kagera (TASEKA)
wakati akitolea ufafanuzi malalamiko yanatolewa na baadhi
ya wakandarasi wanaodai kuwa zabuni za ujenzi wa barabara zinatolewa kwa
upendeleo hasa kwa makandarasi wenye uwezo mkubwa.
Bishanga amesema umoja wa
wakandarasi unapokuwa hai unaweza kuleta wawekezaji wenye mitambo mikubwa ya
ujenzi ambayo ambayo wakandarasi wenye uwezo mdogo wanaweza kuikodisha
tofauti na utaratibu wa sasa ambao wakandarasi wanaitumia wa kukodi mitambo
toka kwa makandarasi wenye uwezo mkubwa wanaoshindana nao zinapotangazwa zabuni.
Alisema si
kweli kwamba TANROADS inatoa zabuni za ujenzi wa barabara kwa upendeleo hasa
kwa wakandarasi wakubwa, Bishanga alisema wakala hao wa barabara wanatoa zabuni
kwa kuangalia vigezo vingi.
"Ndugu mwandishi kawaida zabuni ufunguliwa
mbele ya wakandarasi wote wanaokuwa wameomba kazi, zikifunguliwa kila ombi moja
moja uchambulisha hapo ndipo mshindi wa zabuni utangazwa" mhandisi huyo.
"Mimi siwatetei maofisa wa TANROADS wanaogawa zabuni ninachokisema kulingana na uzoefu nilionao
kwamba wanaonyimwa zabuni ni makandarasi wasio na sifa ya kutekeleza miradi ya
ujenzi wa barabara, makandarasi wasio na sifa ni wale wasio na mitaji, vitendea
kazi na wsenye sifa za kutokuwa waaminifu hasa katika kukamilisha kazi
wanazopewa" alisema Bishanga.
Naye Manyus Rweyendelela ambaye pia ni
mkandarasi aliwaomba wakandarasi watimize vigezo vyote vinavyotakiwa wakati wa
kuomba zabuni.
"Sio siri taarifa zinazoenezwa za kuichafua
TANROADS zinaenezwa na makandarasi wanakosa tenda kwqa kushindwa kutimiza
vigezo" Alisema.
"Mimi ni mkandarasi mdogo ila huwa ninaomba
kazi TANROADS, wakati mwingine nakosa wakati mwingine napata, nasema tangu
nianze kuomba zabuni TANROADS sijawahi kutoa rushwa ili nishinde zabuni,
wanaoeneza taarifa za upotoshaji wana mawazo mufilisi" alisema Manyus.
Kwa upande wake Julius Basinda alisema ndani ya
TANROADS hakuna namna mkandarasi anaweza kushinda zabuni kwa kutoa rushwa
siku ya kufungua zabuni kila kitu huwekwa hadharani.
"Ninachosema ushindi wa zabuni ni kutimiza
vigezo, ndugu zangu wakandarasi msijidanganye kwa kufikiri kwamba mtashinda
zabuni kwa maneno au kwa kutumia rushwa hali hiyo ilishabadili siku
nyingi" alimaliza.
SERIKALI YASHAURIWA SHULE ZINAZOIBA MITIHANI
BAADHI ya wadau wa sekta ya elimu
katika mkoa wa Kagera wameishauri serikali kuzifungia kabisa shule zinazobainika
kujihusisha na wizi wa mitihani pamoja na kuwachukulia hatua za kali
baadhi wamiliki wa shule hizo na maofisa wa serikali
wanaoshirikiana nao ili iweze kukuza na kuimarisha sekta hiyo nchini.
Wadau sekta hiyo wametoa ushauri huo
leo kwa nyakati tofauti wakati wakieleza sababu mbalimbali zinazochangia
kudumaza ukuaji wa kiwango cha elimu hapa nchini.
Walisema kushuka kwa kiwango cha
elimu hapa nchini kunachangiwa na tabia ya kuvuja kwa mitihani, walisema
kuvuja kwa mitihani kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya
wamiliki wa shule binafsi ambao hupenda shule zao zionekane maarufu zaidi
ya shule nyingine.
Mwandishi maarufu wa vitabu hapa
nchini vinavyohusiana na masuala ya kilimo Pius Ngeze ambaye pia ni
mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha mapinduzi (CCM) wa mkoa wa Kagera
alisema wamiliki wa shule wanaoshirikiana na baadhi ya maofisa wa baraza la
mitihani kuiba mitihani kwamba wanaua nchi.
Ngeze aliwafananisha ya
wamiliki wa shule wanaowapa majibu wanafunzi ili shule zao zionekane zinafanya
vizuri sawa na wauwaji, alisema mmiliki wa shule anayewampa wanafunzi majibu ya
mtihani ili shule yake ionekana inafanya vizuri kuwa anakuwa anawamchimbia kaburi.
Leonidas Mgashe, ambaye ni
afisa utalii wa kampuni ya utalii ya walkgard iliyoko mkoani Kagera anasema kuna
baadhi ya wamiliki wa shule binafsi wanaotaka shule zao zionekane maarufu
zaidi ya shule nyingine, aliwatuhumu kuwa wamiliki hao ndio wanajihusisha na
vitendo vya wizi wa mitihani ili shule zao zifanye vizuri waweze kupata wateja
wengi zaidi.
Naye, mwenyekiti wa baraza la
usafiri wa majini na nchi kavu mkoani Kagera, Michael Cleophace alitoa ushauri
kwa watendaji wa baraza la mitihani
kuzingatia maadili ya kazi yao ili
wajiepushe na vishawishi waweze kuinua na kuimarisha kiwango cha elimu hapa
nchini.
Alimaliza kwa kuiomba serikali kubuni
mikakati itakayosaidia kuthibiti mianya yote inayochangia kuvuja kwa mitihani
inayotungwa na baraza la mitihani.
Tuesday, April 23, 2013
KIKAO CHA MABALOZI WA AFRIKA JUMUIA YA ULAYA
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala
akiongoza Mkutano wa Mabalozi wa Afrika Jumuiya ya Ulaya wa kujadili
changamato za uanzishwaji wa Mfuko wa Kijani wa Mazingira Duniani.
MKE WA WAZIRI MKUU AKUTANA NA WATOTO DODOMA
Watoto wa Kijiji cha matumaini cha Mjini Dodoma wakifurahia zawadi ya
asali waliyopewa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (mwenye miwani
katikati) wkati alipotembelea kijiji hicho Aprili 23,2013.Kulia kwake ni
Mbunge wa Viti Maalum na Mkurugenzi wa Mfuko wa Catherine Foundation
Limite, Catherenie Magige ambaye pia alitoa zawadi mbali mbali kwa
watoto wa kijiji hicho.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mmoja wa watoto wa kijiji cha Matumaini cha Dodoma akifurahia pipi ambayo iliku ni miongoni mwa zawadi nyimgi za vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolwa na Mke wa Waziri mkuu, Mama Tunu Pinda na Mbunge wa Viti Maalu, Catherine Magige ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Catherene Foundation kwa watoto wa kijiji hicho, Aprili 23, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (mwenye miwani katikati) na Mbungewa Viti Maalum na Mwenyekiti wa Mfuko wa Catherene Foundation, Caherine Magige wakizungumza na watoto wa kijiji cha Mtumaini cha Dodoma wakati walipotoa zawadi za vyakula na vitu mablimbali kwa kituo hicho, Aprili 23, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mmoja wa watoto wa kijiji cha Matumaini cha Dodoma akifurahia pipi ambayo iliku ni miongoni mwa zawadi nyimgi za vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolwa na Mke wa Waziri mkuu, Mama Tunu Pinda na Mbunge wa Viti Maalu, Catherine Magige ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Catherene Foundation kwa watoto wa kijiji hicho, Aprili 23, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (mwenye miwani katikati) na Mbungewa Viti Maalum na Mwenyekiti wa Mfuko wa Catherene Foundation, Caherine Magige wakizungumza na watoto wa kijiji cha Mtumaini cha Dodoma wakati walipotoa zawadi za vyakula na vitu mablimbali kwa kituo hicho, Aprili 23, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Monday, April 22, 2013
HAYA NI MAMBO YA UCHUMBA
Binti yake mhandisi Timoth Zelamula akimtambulisha mme wake mtarajiwa wakati wa kuvalishana pete, sherehe ya uvalishanaji wa pete ilienda sambamba na utolewaji wa maali.
Sunday, April 21, 2013
RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA TUSKON
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda la Uturuki (TUSKON) Bw. Rizanur Meral na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam.
PICHA NA IKULU
Friday, April 19, 2013
BALOZI SEFUE AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazungumzo na balozi wa
Uingereza nchini Tanzania Mhe Diana Melrose aliyemtembelea leo April 19,
2013
ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam. mazungumzo hayo yalihusu maswala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue akisalimiana na Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Uingereza
(DFID) nchini Bw. Elliot Marshall aliyeongozana na Balozi wa Uingereza
nchini Tanzania Mhe Diana Melrose (katikati) aliyemtembelea leo April 19,
2013 ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam. mazungumzo hayo yalihusu
maswala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.BALOZI KAMALA AKUTANA NA MAOFISA WA MAHAKAMA YA KIMATAIFA
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Kamala (Mwenye miwani)
akiwa na Katibu Mkuu wa Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi Mhe. Hugo
Siblesz.
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Kamala akisalimiana na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Yugoslavia Mhe. Serge Brammertz.
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Kamala akisalimiana na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Yugoslavia Mhe. Serge Brammertz.
Wednesday, April 17, 2013
RAIS MSTAAFU AONGELEA SUALA LA KUCHINJA MIFUGO
Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati alipozungumzia suala uhalali wa kuchinja ambalo limekuwa ni gumzo sana hapa nchini kwa kipindi cha hivi karibuni.
WAZIRI MKUU MKOANI DODOMA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Ludewa, Deo
Filikunjombe kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 17, 2013.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 17, 2013. Kutoka kushoto ni Frlister Bura, Leticia Nyerere na Christowaja Mtinda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwene ukumbi wa Spika mjini Dodoma Aprili 17,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 17, 2013. Kutoka kushoto ni Frlister Bura, Leticia Nyerere na Christowaja Mtinda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwene ukumbi wa Spika mjini Dodoma Aprili 17,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA BALOZI WA OMAN
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania
Mhe Yahya bin Moussa al Bakari ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam
leo.
Mazungumzo hayo yalihusu mambo mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi mbili hizi.
PICHA NA IKULU
RAIS KIKWETE NCHINI UHOLANZI
Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete katika ofisi yake na kufanya naye mazungumzo jana Jijini The
Hague.Rais Kikwete alikuwa katika ziara rasmi ya siku mbili nchini Uholanzi
kwa mwaliko wa Waziri mkuu wa Nchi hiyo.*
**
*Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati alipokuwa
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa ziara yake
rasmi ya siku mbili nchini Uholanzi jana.Kulia nia Waziri Mkuu wa Uholanzi
Mh.Mark Rutte(picha na Freddy Maro).
Subscribe to:
Posts (Atom)