Monday, February 11, 2013

WATALII 22 TOKA UHOLANZI WAISHUKURU KAMPUNI YA UTALII YA KIROYERA YA KAGERA


 Baadhi ya vivutio vya utalii vilivyotembelewa na waholanzi.

Kampuni ya Utalii ya KIROYERA TOURS imeandikiwa barua pepe ya kuwashukuru kwa huduma na mipangilio mizuri ya watalii 22 kutoka uholanzai walioomba huduma ya kampuni ya utalii ya kiroyera ya kuwaongoza kutoka msaka uganda, Bukoba, malazi hapo Bukoba, meli kwenda Mwanza, safari kwenda serengeti, ngorongoro, hadi Arusha wakiongozwa na Bw William Rutta akijulikana sana kwa jina la Willy Kiroyera. 

Mmoja wa wageni alisema Bukoba is very clean town compared to other town in Uganda!! hongera Mkuu wa mkoa kwa campaign ya usafi

Watalii hao walikua na kampuni bingwa ya kutoka Uholanzi ambayo ina makao yake Nairobi ikijulikana kwa jina la Baobab wakiwa na gari kubwa kitaaalamu inajulikna kama overland truck yenye huduma zote ikiwa meza ndani ya gari, flidge, store ya vyakula , mahema, majiko, maji nk.

Hujumbe wao ulisema hivi ' We all loved good logistics and guiding of kiroyera tours for last six days from uganda all the way to Bukoba, Mwanza and great spot in Serengeti William is great guide Donkewell"

Pamoja na hilo watalii hao walifutahia mji wa Bukoba kwa usafi na kuwa kandokando ya ziwa linapamba mji wa Bukoba. Wakiwa Bukoba walifanya walking tour na bicycle tour pia walilala katika hotel inayomilikiwa na KCU inayojulikana Bukoba coorp hotell na hotel nyingine ya Fios mimi. Tour hii ilianza tarehe 31 Jan na kumalizika tarehe 8 ferb Arusha.

Kampuni ya kiroyera tours inaomba sana wajasiliamali waliokuwa katika biashara ya huduma kama vile guest house, hotel, bar, wasafirishaji kuajiri watoa huduma wenye uwezo mzuri wa kuhudumia wateja ili wageni wakija katika mji wetu waendelee kukaa kwa muda na hiyo itakuwa imechangia uchumi wa mkoa wetu.


 

No comments:

Post a Comment