MIKOA ya Kagera na Kigoma imezindua rasmi mihtasari ya somo la Dini na Maadili litakalofundishwa kuanzia shule za
awali, msingi sekondari hadi vyuo vikuu.
Mihtasari
hiyo imezinduliwa rasmi na UMAKA (Umoja
wa Madhehebu Kagera) wakishirikiana na serikali baada ya mihtasari hiyo
kupitishwa rasmi na Kamishina wa Elimu ili isambazwe katika shule zote tayari
kwa kutumika kufundishia wanafunzi katika ngazi mbalimbali.
Somo
la Dini na Maadili limerasimishwa rasmi kufundishwa shuleni na vyuoni baada ya
UMAKA kuona umuhimu wa kuwa na mihtasari ambayo ni rasmi na inayotambuliwa na
serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili itumike kufundishia
watoto pia na kutahiniwa kama masomo mengine.
Umoja
wa Madhehebu Kagera (UMAKA) ulianzisha
mchakato wa kuandaa mihtasari ya somo la Dini na Maadili
wakishirikiana na serikali ili somo hilo liwe na mihtasari inayofanana katika
kufundishia wanafunzi kuliko hapo awali ambapo somo hilo halikuwa na mihtasari
ya kufundishia.
Kupitia
somo la Dini na Maadili, wanafunzi watafunzwa
maadili mema ya kupendana na kuwapenda watanzania wenzao, kujenga jamii yenye
kuwajibika na kumcha Mwenyezi Mungu bila kujali tofauti za ki-imani kwao, pia
kulelewa na kukua katika malezi ya kufuata sheria na utawala bora.
Serikali
katika kuboresha utumiaji wa Mihtasri mipya ya somo la Dini na Maadili imeagiza
somo hilo likaguliwe na wakaguzi wa serikali pamoja na walimu wakuu wa shule
kama masomo mengine na kutahiniwa katika ngazi zote hadi ile ya taifa.
Pia
katika kuona umuhimu wa somo la Dini na Maadili kufundishwa shuleni, serikali
imeamua mihtasari ya somo hilo itumike Tanzania nzima badala ya Mikoa ya Kagera
na Kigoma walioshirikiana na serikali kuandaa mihtasari hiyo ili wanafunzi wote wa Tanzania wafunzwe dini
na maadili ya kitanzania.
UMAKA
ilianzishwa miaka ya 1980 ikiwa na lengo la kushirikiana na Serikali na
kushauri masuala mbalimbali yahusuyo maadili, amani, usalama na maendeleo ya
jamii ya watanzania. UMAKA inajumuisha
Balaza la Maaskofu Tanzania (TEC),
Balaza la Waislam Tanzania (BAKWATA), na Baraza la Wakristo Tanzania
(CCT).
No comments:
Post a Comment