Wednesday, February 20, 2013

MEYA WA MANISPAA YA BUKOBA AKALIA KUTI KAVU ABURUZWA MAHAKAMANI

BAADHI ya madiwani  wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba wamemburuza mahakamani Mstahiki Meya wa manispaa hiyo Anatory Amani kwa kile kinachodaiwa kuwa alipeleka mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14 Dodoma bila madiwani kuijadili.

Madiwani wa manispaa hiyo waliomburuza mahakamani bila kutaja majina yao wamesema meya huyo amekiuka kanuni zinazowaongoza madiwani, wamesema hatua ya meya huyo ya kupeleka bajeti hiyo bila kujadiliwa inaonyesha jinsi gani anavyowaburuza.

Wakiongea kwa nyakati tofauti walisema sababu kubwa iliyomfanya meya huyo asiitishe kikao cha kujadili bajeti kuwa inatokana na msimamo wa madiwani wa kutaka kumng'oa, walisema alifikiri kuwa kama angeitisha kikao wadiwani wangeshikilia msimamo wao wa kumpigia kura za kutokuwa na imani naye.


Walisema alifanya hivyo kukwepa maswali ambayo angeulizwa na madiwani wanaotaka kumng'oa, waendelea kusema kuwa meya huyo atakiwi japokuwa anataka kungan'gania madaraka,"madiwani hatumtaki kabisa ndio maana anatukwepa, tutamg'oa lazima" alitamba mmoja wa madiwani wanaompinga.

"Sisi hatuna imani naye kabisa tumeishamstukia hata miradi yote anayotaka kutekeleza ndani ya manispaa ya Bukoba anaibuni kwa maslahi yake aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa soko, standi kuu ya mabasi Kyakailabwa, ujenzi wa jengo la kitega uchumi, tumeishamshtukia takuibii tena" alisema mmoja wa madiwani.

By. Furgence Ishenda

No comments:

Post a Comment