TUNAPOONGELEA
mikoa ambayo imekumbana na majanga mengi hapa nchini Tanzania ambayo
yameleta athari nyingi za kijamii na kiuchumi hatupaswi kuusahau mkoa wa
Kagera.
Mkoa
wa Kagera ambao umepakana na nchi za Rwanda, Uganda na Burundi umekuwa chimbuko
la majanga mengi yanayojitokeza hapa nchini ambayo uanzia nchi jirani na
hatimaye kusambaa nchini kote.
Tunaposema
tunapoongelea suala la majanga hatupaswi kuusahau ugonjwa wa UKIMWI ambao kwa Tanzania
ulijitokeza kwa mara ya Kwanza mkoani Kagera kabla ya kusambaa nchini kote,
ulitokea nchini Uganda.
Janga la UKIMWI lilitokea nchini Uganda na
hatimaye likatinga mkoani Kagera, ugonjwa wa UKIMWI ulipoingia mkoani Kagera
kwa mara ya Kwanza ulikuwa ukiitwa jina la ‘Juliana’ .
Jina
la juliana lilitokana na mashati yaliyokuwa yamechorwa nembo ya ndege mgogoni
na kifuani yaliyokuwa yakiingizwa kwa njia ya magendo na wafanyabiashara
watanzania waliokuwa wakifanya biashara na waganda maeneo ya Rukunyu.
Janga jingine lililoukumba mkoa wa
kagera ni lile la uvamizi uliofanywa na Rais wa zamani wa Uganda Nduli Idd Amin
mwaka 1979, uvamizi huo ulileta madhara makubwa ambayo ni pamoja na vifo vya
watu wengi pia ulichangia kudumaza maendeleo ya uchumi na kijamii nchini
Tanzania.
Mbali na majanga yote hayo sasa kuna janga
jingine jipya lililojitokeza mkoani humo ambalo limeanza kuonyesha athari
nyingi ambazo ni pamoja na kiuchumi na kijamii, janga hilo sio jingine bali ni la
ugonjwa wa mnyauko wa migomba unaojulikana kwa jina maarufu kwa jina la
unyanjano.
Ugonjwa wa mnyauko umeanza kuhatarisha
usalama wa zao la ndizi ambalo ndilo zao kuu la chakula na biashara katika mkoa humo
hii inafutia hatua ya ugonjwa huo kusambaa kwa kasi ya ajabu.
Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa unyanjano
uzalishaji wa ndizi mkoani Kagera umekuwa ukipungua kila kunapokucha, migomba
mingi mkoani humo imeathirika sana na ugonjwa huo ambao unaonekana kuwa
tishio.
Mkoani Kagera wilaya ambazo
zimeathirika zaidi kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa unyanjano ni pamoja na
wilaya ya Muleba, Kyerwa, Karagwe, wilaya hizi ndizo uzalisha ndizi kwa wingi ambazo uuzwa
kwenye magulio na masoko mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera, maeneo ya
mikoa mingine iliyoko hapa nchini na nje ya nchi.
Mtafiti mkuu wa chuo vha utafiti wa mazao cha maruku
Innocent Ndyetabula anaelezea athari zinazochangiwa na ugonjwa vwa mnyauko,
anasema kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo hali ya upatikanaji wa ndizi
kwenye masoko na magulio umekuwa mdogo sana.
Ndyetabula anasema kwa sasa kwenye magulio na
masoko mbalimbali yaliyoko mkoania Kagera bei ya ununuzi wa ndizi ni wastani wa
bei kati ya shilingi kati ya 13,000 hadi
30,000.
Anasema kabla ya kuzuka kwa ugonjwa wa mnyauko
wa migomba bei ya ununuzi wa ndizi kwenye masoko na magulio ilikuwa na wastani
wa bei kati ya shilingi 2,500 hadi 8,000 kwenye masoko na magulio na wastani
wa bei kati ya shilingi 1,000 hadi 4,000 toka kwenye mashamba ya wakulima.
Anaendelea kusema kuwa upanda kwa bei ya
ununuzi wa ndizi kwenye masoko na magulio umewafanya wakazi wa mkoa wa Kagera
waliokuwa wanaona ndizi kama chakula chao kikuu waione ndizi sawa na mama mkwe
, kwa sasa ni wahaya wachache wanaoweza kumudu bei ya sasa ya ununuzi wa
ndizi.
Ndyetabula anasema ugonjwa wa mnyauko
umewafanya wahaya wabadili fikira zao, kwa sasa wahaya wanaona vyakula
vyote vinavyoonekana mbele yao bila kufanya uchambuzi, wahaya sasa wanakula
wali, ugali na vyakula vingine ambavyo walikuwa hawavitumii hapo awali.
No comments:
Post a Comment