Kufuatia hatua ya marais wa baadhi ya nchi zinazounda jumuia
ya Afrika Masharik, Kaguta Mseveni, Paul Kagame na Uhuru Kenyatta ya kufikia
makubaliano ya matumizi ya vitabulisho vya uraia kutumika badala ya Passport na
masuala ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya bandari baadhi wananchi mkoani Kagera wametoa maoni yao juu ya
uamzi huo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wamesema uamzi wa viongozi hao
unaashiria kuvunjika kwa mara ya pili kwa jumuia ya afrika mashariki , jumuia
ya kwanza iliyokuwa imeimarika kiuchumi ilivunjika mwaka 1977, ambayo ilifuatia
mismamo tofauti ya marais wa nchi waliokuwa wananchama ambao ni pamoja na
hayati mwalimu, julias Nyerere, Idd Amin na Jomo Kenyatta.
Wananchi hao wanasema kiama cha jumuia ya sasa kinakaribia
kwa kuwa kuna masuala ambayo Tanzania kamwe haitakubali yaingie kwenye masuala
ya kiitifaki ya jumuia hiyo ambayo nia pamoja na suala la ardhi.
Wanaendelea kusema kuwa nchi nyingi zilitegemea ardhi
inayomilikiwa na nchi za jumuia hiyo kuwa itakuwa mali ya nchi wanachama, hali hiyo
ingewawezesha wananchi wa jumuia hiyo toka nchi moja kwenda nyingine kutafuta
ardhi.
Tanzania ni moja ya nchi yenye ardhi kubwa miongoni mwa nchi
hizo, hivyo kila nchi inatafuta namna ya kunufaika na ardhi ya nchi yetu, uamzi wa viongozi wa nchi Tanzania wa kutokubali kuiachia ardhi ndio unawaudhi baadhi viongozi wa nchi wanachama.
Nchi nyingi za jumuia hiyo zina ardhi ndogo ambayo hazikidhi
matakwa ya wananchi wa nchi hizo kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji,
walitoa ushauri kwa Rais Jakaya Kikwete akiganganie nchi yetu iwe mmoja wan chi za jumuia ya afrika mashariki,
walishauri aiondoe nchi yetu.
Walisema baadhi ya viongozi wa nchi jumua ya afrika mashariki walilenga zaidi kukopa
rasilimali zinazopatikana katika nchi hii, propoganda zote hizo ni baada ya kuona mipango yao
kukopa rasilimali zilizoko katika nchi imekwama, ndio sasa zinatafuta namna ya kuitenga Tanzania kama namna ya kuitisha itekeleze matakwa ya viongozi wa nchi hizo.
No comments:
Post a Comment