Sunday, October 13, 2013

PICHA ZA MATUKIO YA RAIS KIKWETE KUWASILI MKOANI IRINGA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Iringa jioni ya leo, Jumapili, Oktoba 13, 2013, kwa ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani Iringa. Rais Kikwete amefuatana na Mama Salma Kikwete.
            Shughuli kubwa ambazo Mheshimiwa Rais atazifanya wakati wa ziara hiyo ni kushiriki Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa mgeni rasmi katika Kilele cha Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu wa 2013 na Kilele cha Wiki ya Vijana.
Ndege iliyombeba Rais Kikwete ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa kiasi cha saa 12.20 jioni na kulakiwa na umati mkubwa wa wananchi wakiwemo wafuasi wa vyama vya siasa vikiwamo CCM na Chadema.






No comments:

Post a Comment