Jeshi la Jamhuri ya Demokrasi ya
Congo linasema limeikomboa miji miwili mengine kutoka kwa wapiganaji wa
M23, karibu na mpaka wa Rwanda.
Jeshi liliwaambia waandishi wa habari kwamba
Jumapili limeteka Rutshuru na Kiwanja, katika jimbo la Kivu kaskazini;
baada ya kuteka Kibumba Jumamosi.Umoja wa Mataifa unasema mwanajeshi mmoja wa Tanzania, katika kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, aliuwawa Kiwanja, akijaribu kuwalinda raia.
Mapigano yalizuka Ijumaa, siku chache baada ya mazungumzo ya amani ya mjini Kampala, Uganda, kuvunjika..
Jeshi DRC linadai kuelekea ngome ya M23
Ripoti kutoka Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo zinaeleza kuwa mapigano bado yanaendelea kwa siku ya
tatu huku jeshi la serikali likidai kuwa limeuteka mji wa Kibumba,
mashariki mwa nchi, na kuwatoa wapiganaji wa kundi la M23.
Kibumba, ilioko kilomita 20 kaskazini ya Goma,
ndiko walikokimbilia wapiganaji baada ya kikosi cha Umoja wa Mataifa,
MONUSCO, kuwatoa katika mji wa Goma.Msemaji wa jeshi anaarifiwa kueleza kuwa wameteka miji mengine piya na kwamba jeshi limejigawa na linaelekea kusini upande wa Rutshuru.
Mapigano yalizuka Ijumaa siku chache baada ya mazungumzo ya amani ya mjini Kampala, Uganda, kuvunjika..
No comments:
Post a Comment