Wananchi katika manispaa ya Bukoba wanasubili kwa hamu
taarifa ya timu ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ambayo inachunguza
matumizi mabaya ya madaraka inayomhusu meya wa manispaa ya Bukoba Bw. Anatory
Amani.
Timu hiyo ya CAG baada ya kumaliza kazi yake ya uchunguzi inatarajia
kuwasilisha taarifa hiyo kwa waziri mkuu Mizengio Pinda ambayo baadae itasomwa
mbele ya kikao maalumu cha baraza la madiwani.
Taarifa hiyo ndio itatoa mwelekeo sahihi wa tuhuma zilizokuwa zinaelekezwa kwa meya huyo ambazo ziliwalazimu madiwani wakiongozwa na balozi khamis Kagasheki wafikie hatu ya kusaini waraka wa kutaka kupiga kura za maoni za kumg,oa.
Katika manispaa ya Bukoba baadhi ya madiwani wameahidi kutohudhuria
vikao vitakabyoitishwa na meya huyo hadi taarifa ya CAG itakaposomwa mbele yao
na kudhihirisha ukweli wa tuhuma wanazozielekeza kwa meya Amani.
Madiwani wa manispaa ya Bukoba wanadai meya anawazunguka kwa
kuingia kwenye mikataba bila kuwashirisha, mikataba iliyoingiwa ambayo madiwani
hao wana mashaka nayo ni pamoja na ulw
wa ujenzi wa soko jipya la Bukoba.
Wanaitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na upimaji wa
viwanja 5,000, ujenzi wa standi kuu ya mabasi eneo la Kyabailabwa, ujenzi wa
jengo la kitega uchumi standi ya mabasi ya zamani, mikopo toka TIB na miradi
mingine mingi.
Madiwani hao wanadai hadi kieleweke, inaonekana hawana tena
hamu na meya huyo kwa kuwa mpango wao mzima ni kutaka kumg,oa.
No comments:
Post a Comment