Rais wa Malawi, Joyce Banda amelifuta kazi baraza lake la mawaziri kutokana na kuongezeka kwa visa vya ufisadi serikalini.
Maafisa wa serikali wamekuwa wakipatikana na
pesa zikiwa zimefichwa chini ya vitanda vyao na kwenye magari yao, kwa
mujibu wa mwandishi wa BBC Raphael Tenthani.Wahisani wa kimataifa wamekuwa wakimtaka rais Banda kuchukua hatua kukabiliana na ufisadi.
Malawi ni taifa masikini na hutegemea sana msaada kutoka kwa Muungano wa Ulaya na nchi zengine za kimagharibi.
Bi banda amesema kuwa mawaziri wapya watateuliwa hivi karibuni bila ya kutoa maelezo zaidi.
Aliitisha mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri kabla kutangaza kulivunja.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari Banda alisema kuwa ameunda jopo maalum likijumuisha polisi na maafisa wa serikali kufanya ukaguzi wa matumizi ya pesa za serikali katika idara zote za serikali.
Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kupigwa risasi kwa bwana Mphwiyo ndio ilikuwa mwanzo wa taarfa kuwa baadhi ya maafisa wa serikali wanashirikiana na wafanyabisahara kuifilisi serikali katika utoaji wa kandarasi na mikataba bandia.
Washukiwa wanne walikamatwa kuhusiana na kupigwa risasi kwa afisa huyo.
Takriban maafisa kumi wa serikali wama
ekamatwa wakisubiri kusikilizwa kwa kesi zao kuhusiana na ufisadi.
No comments:
Post a Comment