Thursday, October 31, 2013

Uhuru wa vyombo vya habari hatarini Kenya


Wabunge amepitisha mswaada utakaodhibiti vyombo vya habari Kenya
Wabunge nchini Kenya wamepitisha mswaada utakaopelekea kuidhinishwa kuundwa kwa jopo maalum litakalodhibiti uhuru wa vyombo vya habarinchini humo.
Mswdaa huo utalipa jopo mamlaka kuwaadhibu vikali wanahabari watakaosemekana kuvunja sheria na kukiuka maadili ya utenda kazi kwa kuwatoza viwango vikubwa vya faini.
Wamekubali kumtoza faini ya zaidi ya dola laki mbili mwandishi habari yeyote atakayevunja sheria au shilingi milioni 20 za Kenya kwa kukiuka maadili ya kazi.
Ikiwa mwandishi atakosa uwezo wa kulipa faini hiyo, basi jopo hilo pia lina mamlaka ya kuuza mali yake ili kupata pesa hizo.
Wabunge hao inaarifiwa walipitisha kwa haraka mswaada huo wa kubuni jopo litakaloteuliwa kisiasa ili kuwaadhibu vikali waandishi wataosemekana kukiuka sheria.
Hata hivyo sheria hii inasemekana kuwa moja ya sheria mbaya zaidi za kukandamiza vyombo vya habari kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.
Mswaada huo unaipa serikali mamlaka ya kumwondoa mwandishi wa habari katika sekta hiyo, inaweza kufanya msako katika afisi za vyombo vya habari na kuchunguza akaunti za benki za vyombo hivyo pamoja na zile za waandishi wenyewe.
Jopo hilo linaweza kufanya chochote litakalo kwa sababu linapewa mamlaka makubwa sana na mswaada huo.
Bunge la Kenya linaruhusiwa na katiba kuweka sheria inayodhibiti vyombo vya habari pamoja na kuhakikisha kuwa vinafuata sheria. Lakini katiba hairuhusu serikali hiyohiyo wala wansiasa kusimamia jopo hilo.
Katiba ya Kenya pia hairuhusu serikali kudhibiti vyombo vya habari kwa njia yoyote itakayo.

MANDHALI YA MANISPAA YA BUKOBA






Wednesday, October 30, 2013

Waasi wa M23 watimuliwa Bunagana



Wanajeshi wa DRC wiki hii wamefanikiwa kukomboa maeneo mengine kutoka kwa M23
Wanajeshi wa DRC wamefanikiwa kuwatimua waasi wa M23 kutoka katika ngome yao kuu katika eneo la Bunagana.

Wanajeshi hao wamekomboa mji wa Bunagana kufuatia makabiliano makali adhuhuri ya leo ambapo baadhi ya waasi walilazimika kuimbilia msituni huku baadhi wakidai waliingia Uganda baada ya kuvalia mavazi ya kiraia.
Msemaji wa serikali alisema kuwa mji wa Bunagana ulio katika mpaka wa Uganda na DRC, sasa uko chini ya wanajeshi wa serikali.

Wenyeji wa mji huo walithibitishia BBC kuwa mji huo ulikombolewa na kuwa waasi wamekuwa wakitoroka mapambano makali dhidi yao.

Hatua hii ya wanajeshi ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao wanajeshi wamekuwa wakiupata dhidi ya waasi hao wa M23 walianza harakati zao dhidi ya serikali ya Congo mwaka jana wakidaiwa kusaidiwa na serikali ya Rwanda.

Mnamo siku ya Jumatatu mjumbe maalum wa M23 hawana tena nguvu za kijeshi kwani sio tesho tena.,

Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakimbizi elfu tano wamelazimika kutoroka Bunagana na kuingia Uganda kwa usalama wao.

Tanzania: Tunaweza kujitoa A. Mashariki


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.

Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.
Waziri anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa mkataba wa jumuiya hiyo.

Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.

Kwa mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa pili uliofanyika Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himaya moja ya forodha.

Mambo mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.

Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumzia kuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.

Tayari Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.

RAIS KIKWETE ASHAURIWA MAMBO YA KUNUFAISHA NCHI


Kufuatia hatua ya marais wa baadhi ya nchi zinazounda jumuia ya Afrika Masharik, Kaguta Mseveni, Paul Kagame na Uhuru Kenyatta ya kufikia makubaliano ya matumizi ya vitabulisho vya uraia kutumika badala ya Passport na masuala ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya bandari  baadhi wananchi  mkoani Kagera wametoa maoni yao juu ya uamzi huo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wamesema uamzi wa viongozi hao unaashiria kuvunjika kwa mara ya pili kwa jumuia ya afrika mashariki , jumuia ya kwanza iliyokuwa imeimarika kiuchumi ilivunjika mwaka 1977, ambayo  ilifuatia mismamo tofauti ya marais wa nchi waliokuwa wananchama ambao ni pamoja na hayati mwalimu, julias Nyerere, Idd Amin na Jomo Kenyatta.

Wananchi hao wanasema kiama cha jumuia ya sasa kinakaribia kwa kuwa kuna masuala ambayo Tanzania kamwe haitakubali yaingie kwenye masuala ya kiitifaki ya jumuia hiyo ambayo nia pamoja na suala la ardhi.

Wanaendelea kusema kuwa nchi nyingi zilitegemea ardhi inayomilikiwa na nchi za jumuia hiyo kuwa itakuwa  mali ya nchi wanachama, hali hiyo ingewawezesha wananchi wa jumuia hiyo toka nchi moja kwenda nyingine kutafuta ardhi.

Tanzania ni moja ya nchi yenye ardhi kubwa miongoni mwa nchi hizo, hivyo kila nchi inatafuta namna ya kunufaika na ardhi ya nchi yetu, uamzi wa viongozi wa nchi Tanzania wa kutokubali kuiachia ardhi ndio unawaudhi baadhi  viongozi wa nchi wanachama.

Nchi nyingi za jumuia hiyo zina ardhi ndogo ambayo hazikidhi matakwa ya wananchi wa nchi hizo kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji, walitoa ushauri kwa Rais Jakaya Kikwete akiganganie nchi yetu iwe  mmoja wan chi za jumuia ya afrika mashariki, walishauri aiondoe nchi yetu.

Walisema baadhi ya viongozi wa nchi  jumua ya afrika mashariki walilenga zaidi kukopa rasilimali zinazopatikana katika nchi hii, propoganda zote hizo ni baada ya kuona  mipango yao kukopa rasilimali zilizoko katika nchi imekwama,  ndio sasa zinatafuta namna ya kuitenga Tanzania kama namna ya kuitisha itekeleze matakwa ya viongozi wa nchi hizo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

a Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatatu, Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun.

Mkutano huo wa siku mbili utafanyika keshokutwa Jumatano na Alhamisi kwenye Ukumbi wa Queen Elizabeth 2 mjini London.

Miongoni mwa mambo makuu ambayo mkutano huo utazungumzia ni Serikali Uwazi na Ajenda ya Maendeleo Baada ya Mwaka 2015 wakati muongo wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millenium Development Goals) unafikia mwisho.

Masuala mengine ambayo yatazungumzwa katika mkutano ambao Rais Kikwete anaambatana na Mawaziri wake watatu ni pamoja na uwazi katika manunuzi ya umma, uwazi katika mikataba, haki ya kupata habari, uwazi katika ukaguzi wa fedha za umma, uwazi wa Serikali na vyombo vya habari, uwazi katika mikataba ya maliasili, uwazi katika maendeleo ya nchi zinazoendelea.


Mawaziri wanaoambatana na Rais Kikwete katika ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe, Waziri wa Sheria na Katiba Mheshimiwa Mathias Chikawe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar Mheshimiwa Mwinyihaji Makame.

Rais Kikwete anatarajia kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 2, 2013.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Oktoba, 2013

RAIS JK AENDA UINGEREZA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Swissport katika uwanja wa ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere wakati akielekea kwenye ndege jioni ya jana, Jumatatu, Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe na Meneja wa Shirika la ndege la Emirates uwanjani hapo Bw. Aboubakar Jumaa. (PICHA NA IKULU)

Monday, October 28, 2013



Wananchi katika manispaa ya Bukoba wanasubili kwa hamu taarifa ya timu ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ambayo inachunguza matumizi mabaya ya madaraka inayomhusu meya wa manispaa ya Bukoba Bw. Anatory Amani.

Timu hiyo ya CAG baada ya kumaliza kazi yake ya uchunguzi inatarajia kuwasilisha taarifa hiyo kwa waziri mkuu Mizengio Pinda ambayo baadae itasomwa mbele ya kikao maalumu cha baraza la madiwani.

Taarifa hiyo ndio itatoa mwelekeo sahihi wa tuhuma zilizokuwa zinaelekezwa kwa meya huyo ambazo ziliwalazimu madiwani wakiongozwa na balozi khamis Kagasheki wafikie hatu ya kusaini waraka wa kutaka kupiga kura za maoni za kumg,oa.

Katika manispaa ya Bukoba baadhi ya madiwani wameahidi kutohudhuria vikao vitakabyoitishwa na meya huyo hadi taarifa ya CAG itakaposomwa mbele yao na kudhihirisha ukweli wa tuhuma wanazozielekeza kwa meya Amani.

Madiwani wa manispaa ya Bukoba wanadai meya anawazunguka kwa kuingia kwenye mikataba bila kuwashirisha, mikataba iliyoingiwa ambayo madiwani hao wana mashaka nayo  ni pamoja na ulw wa ujenzi wa soko jipya  la Bukoba.

Wanaitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na upimaji wa viwanja 5,000, ujenzi wa standi kuu ya mabasi eneo la Kyabailabwa, ujenzi wa jengo la kitega uchumi standi ya mabasi ya zamani, mikopo toka TIB na miradi mingine mingi.

Madiwani hao wanadai hadi kieleweke, inaonekana hawana tena hamu na meya huyo kwa kuwa mpango wao mzima ni kutaka kumg,oa.

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA MJANE NA FAMILIA YA BALOZI ISAAC SEPETU LEO

 :Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa wanafamilia wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki jana  jijini Dar es salaam.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 




Sunday, October 27, 2013

RAIS KIKWETE MGENI RASMI JUBILEI YA MIAKA 100 YA PAROKIA YA LUGOBA

Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika  Parokia ya Lugoba, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, leo Oktoba 27, 2013 wakati wa sherehe za Jubilei ya Miaka 100 wa Parokia hiyo.i ya Miaka 100 wa Parokia hiyo.


PICHA NA IKULU

Jeshi la DRC lakomboa miji mitatu


Mpiganaji wa M23 Rutshuru
Jeshi la Jamhuri ya Demokrasi ya Congo linasema limeikomboa miji miwili mengine kutoka kwa wapiganaji wa M23, karibu na mpaka wa Rwanda.
Jeshi liliwaambia waandishi wa habari kwamba Jumapili limeteka Rutshuru na Kiwanja, katika jimbo la Kivu kaskazini; baada ya kuteka Kibumba Jumamosi.
Umoja wa Mataifa unasema mwanajeshi mmoja wa Tanzania, katika kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, aliuwawa Kiwanja, akijaribu kuwalinda raia.
Mapigano yalizuka Ijumaa, siku chache baada ya mazungumzo ya amani ya mjini Kampala, Uganda, kuvunjika..


Jeshi DRC linadai kuelekea ngome ya M23


Mwanajeshi wa serikali na ushanga wa risasi, karibu na KIbumba
Ripoti kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinaeleza kuwa mapigano bado yanaendelea kwa siku ya tatu huku jeshi la serikali likidai kuwa limeuteka mji wa Kibumba, mashariki mwa nchi, na kuwatoa wapiganaji wa kundi la M23.
Kibumba, ilioko kilomita 20 kaskazini ya Goma, ndiko walikokimbilia wapiganaji baada ya kikosi cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO, kuwatoa katika mji wa Goma.
Msemaji wa jeshi anaarifiwa kueleza kuwa wameteka miji mengine piya na kwamba jeshi limejigawa na linaelekea kusini upande wa Rutshuru.
Mapigano yalizuka Ijumaa siku chache baada ya mazungumzo ya amani ya mjini Kampala, Uganda, kuvunjika..

Saturday, October 26, 2013

MAHAFALI YA 39 YA SHULE YA SEKONDARI YA KISHOJU

 Ayesiga kulia na Kalumuna Ivan kushoto.
 Mkuu wa wilaya ya Muleba Lembres Kipuyo akiteta jambo na Geofrey, Diwani wa kata ya Magatta Kalutanga wakati wa mahafali ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya Kishoju na harambee ya kutunisha mfuko wa kukarabati miundo mbinu ya shule hiyo.
 Baadhi ya wanafunzi wahitimu.



Kipuyo akihutubia.

RAIS KIKWETE IKULU


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Pakistan nchini Mhe Tajammul Altac aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 26, 2013 kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa  Pakistan nchini Mhe Tajammul Altac aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 26, 2013 kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi.

PICHA NA IKULU

Serikali Kikwazo-Zitto Kabwe



Wakati shinikizo la Dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la ukwepaji kodi na Utoroshaji wa fedha kutoka nchi za Kiafrika, serikali ya Tanzania inavuta miguu.

Moja ya njia ya Serikali za nchi maskini kupata taarifa za makampuni makubwa ya kimataifa(MNCs) yanayokwepa kodi ni mfumo wa kupashana taarifa (automatic exchange of tax information) .

Kufutia shinikizo la nchi mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa "secrecy jurisdictions" (tax havens) Zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa taarifa. Tanzania mpaka sasa haijaweka sahihi na serikali haijatoa taarifa yeyote kwa Umma.
Ghana, Afrika Kusini na Nigeria nchi zinazotegemea sana rasilimali kama Tanzania zimeweka saini mkataba huu tayari. Asilimia 44 ya fedha za kigeni nchini zinatokana na mauzo ya madini nje. Makampuni ya madini ndio yanaongoza kukwepa kodi.

Tanzania inapoteza jumla ya dola za kimarekani kati ya milioni 500 na bilioni 1.25 kwa mwaka kutokana na Makampuni makubwa ya kimataifa kukwepa kodi. Hii ni sawa na kusema Tanzania inapoteza dola takribani milioni mbili kila siku kwa uporaji huu.

Naitaka serikali kutoa taarifa kwa nini haichuki hatua kuzuia mwanya huu wa mapato ya Umma. Serikali ichukue hatua mara moja kuhakikisha Tanzania inaingia makubaliano ya kupashana taarifa za kikodi. Huu sio wakati wa kuvuta miguu katika suala nyeti la umma. Badala ya kukimbilia kutoza kodi wanyonge, tuhakikishe makampuni makubwa yanayonyonya rasilimali zetu yanalipa kodi inayotakiwa.

Zitto Kabwe, MB
Waziri Kivuli wa Fedha

24 Oktoba, 2013
Geneva, Switzerland

WAZIRI MKUU PINDA AZAWADIWA CHINA

Waziri Mkuu, Mizengo PInda kipokeazawadi ya picha  kutoka wa  Gavana wa jimbo la  Guangdong nchini China, Bw. Zhu Xiaodan  baada  ya mazungungumzo yao kwenye hoteli  ya Dong Fang mjini Guanzhou akiwa katika ziara ya kikazi nchini China Oktoba 24, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wednesday, October 23, 2013

MAMBO YA PROFESA TIBAIJUKA

 Waziri wa ardhi, nyumba na makazi na mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka wa pili toka kushoto, akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukagua vitalu vya miti aina ya pine, miti hiyo ni kukijengea uwezo chama cha mapinduzi katika kata ya Kagabilo.


 Jengo la taasisi ya Kajumulo iliyoko eneo Kagabilo, anayeonekana sio mwingine ni Profesa Anna Tibaijuka.
 Sehemu ya mandhari ya taasisi ya Kajumulo, hapa ni sehemu ya jiko.

Profesa Tibaijuka akiwa na mama yake mzazi anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 80.