Tangu uhuru wa iliyokuwa Tanganyika sasa Tanzania mwaka 1961 miaka 53 ya uhuru mkoa wa Kagera
umekuwa ukiongozwa na viongozi mbalimbali hasa katika nafasi ya ukuu wa mkoa na kwa kipindi hicho chote hadi
sasa tayari mkoa umeongozwa na wakuu wa mikoa wapatao 21 kwa vipndi tofauti.
Viongozi hao (Wakuu wa Mkoa) waliowahi kuuongoza mkoa wa Kagera kwa
nyakati tofauti waliweza kuisogeza Kagera kutoka katika hali
fulani na kupiga hatua kimaendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchumi,
elimu, siasa, utamaduni, miundombinu, na
nyanja mbalimbali za ustawi wa jamii.
Mkoa wa Kagera chini ya uongozi
wa Mkuu wa Mkoa wa sasa Mheshimiwa John V.K. Mongella ulimuaga aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa Kagera wa 20 na aliuongoza
mkoa kwa miaka mitatu akiteuliwa
kutoka katikanafasi ya Ukuu wa Wilaya ya Karagwe naye ni Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe kwa jina maarufu Mulokozi.
Kama walivyokuwa watangulizi wake
Mhe. Kanali Mstaafu Massawe alifanya mengi katika mkoa wa Kagera na kuweka
rekodi ya mambo mengi aliyoyafanya yakiongozwa na kaulimbiu yake ya “Amani
na Maendeleo” kubakia katika kumbukumbu za mkoa wa Kagera na
wananchi wake kwa ujumla.
Historia Fupi
Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe kabla ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Kagera alifanya kazi mbalimbali na mahali pengi akiwa na uzoefu mkubwa wa uendeshaji na usimamiaji wa shughuli za
umma. Kabla ya kuwa mwanasiasa amekuwa ni
Afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Mtaaluma na Mwanamichezo.
Alijiunga na
Jeshi la Wananchi Tanzania mwaka 1979 katika cheo cha Luteni Usu na aliendelea
kupandishwa vyeo mpaka cheo cha Kanali alichotunukiwa Januari 2002. Akiwa
Jeshini alihudhuria mafunzo lukuki hadi yale ya High Commander Defence Styles.
Kitaaluma Mhe. Massawe ni Mwalimu
na Mtaalamu wa Maendeleo (Development Studies).
Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Julai 2006, akiwa mtumishi wa umma mwenye
uzoefu mkubwa hasa katika elimu ambapo alikuwa Mkuu wa shule maarufu ya
Jitegemee ya Jijini Dar es Salaam kwa
muda wa miaka 17.
Kwa upande wa michezo Mhe.
Massawe ni hazina kubwa ya uendeshaji na usimamizi wa michezo, aidha aliwahi
kuwa Mkurugenzi wa michezo katika Jeshi la kujenga Taifa, Katibu Mkuu Tanzania
Boxing Association, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Olympiki Kanda ya Tano na
Mjumbe wa Balaza la Michezo Tanzania .
Medali Alizowahi Kutunzwa
Massawe aliwahi kutunzwa medali 8 (nane) za utambuzi kutokana na
mchango wake uliotukuka katika utumishi wa umma. Kwanza, Octoba 1995 Wizara ya
Elimu ilimtunuku cheti cha kuwa Mkuu wa shule bora. Pili, Octoba 1998
alitunukiwa cheti maalum cha utambuzi wa
mchango wake uliotukuka (Excellent contribution) katika kukuza Uskauti nchini kutoka Skauti Tanzania.
Medali ya tatu,
Januari 2002 alipewa hati ya kuutambua mchango wake katika kukuza mchezo wa
handball Afrika Mashariki na Kati. Nne, Januari 2005 alipewa hati na Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki (East African Cooperation) katika kutambua mchango wake
mahiri akiwa kiongozi wa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania katika mashindano
ya kwanza ya michezo na utamaduni ya Majeshi ya Ulinzi ya Afrika Mashariki
mjini Kampala Uganda.
Julai 2011 Mhe. Massawe alipata
cheti kutoka Bodi ya Kahawa Tanzania kwa
mchango wake mkubwa katika kudhibiti magendo ya kahawa katika Wilaya ya
Karagwe. Sita, Machi 2011 Halmashauri ya wilaya ya Karagwe ilimtunuku cheti maalum kwa kuongoza
mafanikio makubwa ya mapambano dhidi ya mimba kwa wananfunzi na Octoba 2011 alipata zawadi kutoka Chuo Kikuu
cha JohnsHopkins cha nchini Marekani kwa
kumlinda mtoto wa kike.
Utumishi wa Umma Kama Mkuu wa
Mkoa
Chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa Mhe. Massawe mkoa uliendelea kuwa
katika hali ya amani na utulivu na aliuacha mkoa ukiwa wenye amani uhakika wa
chakula. Pato la mwananchi lilikuwa shilingi 409,822/- mwaka 2011 aidha aliacha
pato hilo likiwa shilingi 716,209/-
mwaka 2014
Katika kipindi
chake alisimamia mkoa katika usafi na kutunza mazingira ambapo wananchi wa
Manispaa ya Bukoba waliipa siku ya Alhamisi kuwa Massawe Day. Katika Sekretarieti ya Mkoa Mhe. Massawe
alihimiza mambo makuu muhimu yafuatayo:
Amani na na Maendeleo katika
mkoa, alikuwa mstari wa mbele katika kupigana vita dhidi ya maadui 14 ambao ni Malumbano ya kisiasa, Uhamiaji haramu, Wizi
wa kutumia siraha, Mauaji ya albino na vikongwe, Uchukuaji wa sheria mkononi,
Unyanyasaji wa kijinsia, Migogoro ya ardhi na Wizi wa mifugo.
Maadui aliopambana nao Mhe.
Massawe ni pamoja na Biashara ya magendo
ya kahawa, Upachikaji wa mimba kwa watoto wa shule, Ushirikina na upigaji wa
ramli za kichonganishi, Uharibifu wa mazingira na uchomaji moto ovyo, Uzururaji ovyo na ukaaji vijiwni na kunywa
kahawa muda wote wa kazi na unywaji wa pombe saa za kazi.
Mhe. Massawe alihimiza wananchi
kufanya kazi na alijenga serikali ya mkoa yenye kushirikiana na wananchi,
mashirika yasiyokuwa ya serikali madhehebu ya dini pamoja na wadau mbalimbali
wa maendeleo katika mkoa na nje ya mkoa wa Kagera.
Aidha aliwahimiza wananchi
kupendana na kufanya kazi na kuondokana na Kamunobele, Olwango, Kitandugaho,
Etima, Obunafu na Eilangira. Hiyo yote ilikuwa ni kuchochea maendeleo
na ustawi wa mkoa wa Kagera ambao upo katika kitovu cha nchi za Afrika
Mashariki.
Mhe. Massawe akiwa Kagera
alisimamia na kuongoza matukio matukio makubwa ya kitaifa mkoani Kagera, Kwanza
mwaka 2011 Maadhimisho ya Kitaifa ya wiki nenda kwa usalaama barabarani, Miaka
50 ya uhuru Tanzania Bara. Mwaka 2012 Maandalizi ya sensa na makazi ya watu
Mwaka 2013 Mhe. Massawe alisimamia Maadhimisho ya
Siku ya Mashujaa Kitaifa mkoani Kagera, Mchakato wa wananchi kutoa maoni ya
katiba mpya, Maadhimisho ya kitaifa ya Fimbo Nyeupe, Uendeshaji wa Operesheni Kimbunga.
Mwaka 2014 Uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa rekodi kubwa ya
maandalizi.
Mhe. Massawe amekuwa na uhusiano
na mkoa wa Kagera kwa miaka 37 na mara ya kwanza alifika Kagera akiwa Luteni wa
Jeshi la wananchi wakati wa vita vya Nduli Iddi Amini. Aprili 2009 Mhe. Massawe
Akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni alihamishiwa Wilayani Muleba na kuweka rekodi
ya kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo kwa siku
moja na baadae alihamishiwa katika Wilaya ya Karagwe hadi Septemba 2011
alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
ORODHA YA WAKUU WA MKOA WA KAGERA TANGU UHURU MWAKA 1961
Na.
|
JINA LA
MKUU WA MKOA
|
MWAKA
|
1.
|
BW. SAMWEL N. LWANGISA
|
1961 - 1964
|
2.
|
BW. OSWARD MARWA
|
1964 - 1966
|
3.
|
Bw. P. C. WALWA
|
1966 - 1967
|
4.
|
BW. P. C. SEMSHANGA
|
1967 - 1970
|
5.
|
BW. L. N. SIJAONA
|
1970 -1972
|
6.
|
Maj. Gen. TWALIPO
|
1972 -1974
|
7.
|
Brig. M. M. MARWA
|
1974 -1975
|
8.
|
Col. T. A. SIMBA
|
1975 -1977
|
9.
|
Bw. MOHAMED KISOKI
|
1977 -1978
|
10.
|
Capt. PETER KAFANABO
|
1978 - 1981
|
11.
|
Lt. Col. NSA KAISI
|
1981 -1987
|
12.
|
Bw. HORACE KOLIMBA
|
1987 - 1989
|
13.
|
Bw. PAUL KIMITI
|
1989 - 1991
|
14.
|
Capt. A. M. KIWANUKA
|
1991 - 1993
|
15.
|
Bw. PHILIP J. MANGULA
|
1993 - 1996
|
16.
|
Bw. MOHAMMED A. BABU
|
1996 - 1999
|
17.
|
Gen. T. N. KIWELU
|
1999 - 2006
|
18.
|
Col. E. MFURU
|
2006 - 2009
|
19.
|
Bw. MOHAMMED A. BABU
|
2009 - 2011
|
20.
|
Col. (Mstaafu) FABIAN I. MASSAWE
|
2011 - 2014
|
21.
|
Bw. JOHN V.K. MONGELLA
|
2014 -
|
No comments:
Post a Comment