NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
Jeshi la polisi katika mkoa wa KAGERA limeanza kufanikisha
mikakati yake yenye lengo la kusambaratisha mtandao wa watu wasiojulikana
wanaojihusisha na vitendo vya kufadhili na kufanya mauaji ya kuwakata kata watu
kwa MAPANGA na baadae kuwanyonya damu
ambavyo katika kata za KITENDAGULO,
KIBETA na RWAMISHENYE katika manispaa ya BUKOBA.
Katika
kusambatarisha
mtandao huo jeshi hilo limefanikiwa
kuwaua watuhumiwa WAWILI, JOHANES JOSEPH ambaye ni kinara wa mauaji
ya kuwakata kata
MAPANGA na EDWARD THEOPHIL ambao ni miongoni mwa watuhumiwa WANNE
walioshikiliwa kwa tuhuma ya kuhusika na kufadhili vitendo mauaji ya
kuwakata kata
WATU kwa mapanga kwa ajili ya imani za
KISHIRIKINA.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la
polisi mkoani KAGERA, HENRY MWAIBAMBE amesema watuhumiwa waliouwawa kwa kutumia
nguvu za giza walikuwa wakijaribu kuwatoroka maofisa wa jeshi la polisi
waliokuwa wakiwahoji wakati wakiwaonyesha
MAZINDIKO wanayoyatumia katika
kutekeleza mauaji, pamoja na kutoa onyo kwa wanajihusisha na vitendo hivyo pia
amesema jeshi hilo kwamba linamshikilia GAUDENSIA NDIBALEMA ambaye ni mganga wa jadi kwa
tuhuma ya kuwapatia kinga wanajihusisha na vitendo vya mauaji hayo.
CLOUDS TV imefanikiwa
kuongea na baadhi ya wananchi waliolazwa
katika
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa KAGERA walioathrikika kufuatia kukithiri
kwa vitendo hivyo, OMARY HABIB na ALCAD MBELWA ni miongoni mwa waathrika wa
vitendo hivyo wanaoeleza walivyovamiwa na wakata mapanga hao na namna
walivyojinusuru, GETRUDO RUBAKULO ni afisa muuguzi ambaye anaeleza hali ya
waathirika hao, huku muuguzi mkuu wa hospitali ya rufaa BEATRICE KABUNGA takwimu za waliofikishwa hospitalini kwa
kukatwa mapanga katika kipindi cha wiki mbili.
Kufuatia vitendo vya mauaji ya kukata watu kwa mapanga
katika manispaa ya BUKOBA, zaidi ya watu KUMI wameishauwawa , vitendo hivyo
vinahusishwa na imani za kishirikina ambapo inadaiwa kwamba wale wanaokatwa
mapanga damu zao zinavyonywa na kupelekwa pasipojulikana.
For more information contact +255 784 939 586/ 753 844 995
No comments:
Post a Comment