
Shirika la kimataifa la msalaba 
mwekundu limesema kuwa hali inazidi kuwa mbaya nchini Yemen, huku Mji 
mkuu Sanaa ukikosa umeme na maji kwa kipindi cha siku tisa zilizopita.
Afisa
 wa ngazi ya juu wa Shirika hilo nchini humo Robert Mardini amesema 
ameshuhudia miili kadhaa kwenye mitaa alipotembelea mji wa Aden, na 
kueleza kuwa changamoto iliyopo ni upelekaji wa huduma za kitabibu.Awali Saudi Arabia ilisema itaendelea kutumia jeshi kuzuia waasi wa kihudhi kudhibiti Yemen, waasi nao wametaka kumalizwa kwa mashambulizi ya anga dhidi yao na kuanza mazungumzo.
Mpiganaji anayemuunga mkono Rais Abdrabbuh Mansour Hadi amesema ni mapema mno kuanza kuzungumzia makubaliano kati ya pande mbili.
No comments:
Post a Comment