Viongozi wa vyama vitano vya upinzani wameshiriki katika mdahalo wa pili wa moja kwa moja ulioandaliwa na BBC.
Katika
 hoja za kwanza, kiongozi wa chama cha Labour, Ed Miliband, amesema 
suala la familia za wafanyakazi atalipa kipaumbele kwanza, wakati 
kiongozi wa UK Independence Party,UKIP, Nigel Farage amesema atasaidia 
biashara ndogo ndogo. Nicola Sturgeon kiongozi wa chama cha Scotish 
National Party amesema anataka kuona muungano wa Uingereza unakuwa bora 
zaidi katika kila sehemu ya nchi hiyo. Viongozi wa Plaid Cymru na Green 
Party pia nao wameshiriki katika mdahalo huo.Bwana Miliband, amesema anatarajia kupata ushindi mkubwa na hataunda serikali ya mseto na chama cha SNP.
Wagombea hao wamekuwa wakipingana katika masuala mbalimbali wakati wa mdahalo huo.
Waziri mkuu David Cameron wa chama tawala cha Conservatives na naibu waziri mkuu wake kutoka chama cha Lib Dem, Nick Clegg hawakushiriki katika mdahalo huo wa wazi.
No comments:
Post a Comment