Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa
linafanya oparesheni ya mwisho kwenye msitu moja ambao unaaminiwa kuwa
ngome kuu ya wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi (Chris Olukolade) alithibitisha kuwa opaesheni zinaendelea kwenye msitu wa Sambisa karibu na mpaka na Cameroon.Serikali ya Nigeria inasema kuwa Boko Haram wako mbioni na jeshi limeapa kuwashinda kabla ya kuapishwa kwa rais mpya Muhammadu Buhari tarehe 29 mwezi Mei.
Inaaminika kuwa zaidi ya wasichana 200 wa shule ambao walitekwa nyara mwaka mmoja uliopita kutoka mji wa Chibok huenda wameshikiliwa ndani ya msitu huo
No comments:
Post a Comment