Thursday, January 23, 2014

Tikitaka za Mzee Reginald Mengi: Anamiliki share katika makampuni yenye vitalu vya mafuta na gesi.



Katika Mjadala uliofungwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete juu ya suala la Uzawa kwenye utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi hapa nchini. Mjadala huo ambao kwa kiasi kikubwa ulibebwa na pande mbili yaani upande wa Serikali chini ya Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Prof Sospeter Muhongo na upande wa sekta binafsi chini Mzee Reginald Mengi. Tamati ya Mjadala huo ambapo Rais Jakaya Kikwete aliufunga kwa kubainisha kuwa inatosha kwa makampuni ya Serikali kuwawakilisha watanzania katika mchakato wa ushirikishwaji wao katika utafutaji na uvunaji kwa kuwa gharama za mchakato huo ni wa gharama kubwa ambao watanzania wazalendo walio wengi hawana uwezo wa kumudu.

Hitimisho hilo ambalo limekuwa mwiba kwa Mwenyekiti wa Sekta Bnafsi Nchini Bwana Reginald Mengi kwa kuwa si tu ni kiongozi wa sekta binafsi nchini bali pia ni mtu mwenye maslahi ya moja kwa moja na biashara ya utafutaji, uchimbaji na uvunaji wa rasilimali za madini, mafuta na gesi. Hitimisho hilo ni mwiba kwa kuwa hoja aliyoisimamia imeonekana kushindwa mbele ya jamhuri.

Lakini taarifa iliyopatikana punde ambayo ni sahihi, na ambayo imeendelea kuonyesha sarakasi za Mzee Mengi katika suala hilo ni kwamba; Mzee Mengi ni mbia mwenye shares kwa asilimia 3.3 katika kampuni ya watanzania inayofahamika kwa Jina la SWALA ambayo ina blocks 2 za kutafuta mafuta na gesi huko Kilombero  na Pangani. Kampuni hiyo ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Bwana E. Massawe na Mkurugenzi wake Bwana B Mramba.

Taarifa hizi zinaudhihirishia Umma kuwa Mzee Mengi anapigania hoja hii kwa maslahi binafsi na pili inaonyesha ni kwa namna gani amekuwa ni mtu asiyeridhika pamoja na kumiliki sehemu kubwa ya ardhi yenye madini na hata kufanikiwa kupata nafasi katika vitalu vya gesi na mafuta ameendelea kumshutumu Waziri wa Nishati na Madini kwa tuhuma za kutengeneza na hata kumkashifu kuwa ni kiongozi wa Hovyo ambaye anafaa kupelekwa milembe kuangaliwa akili yake.

Kwanza ni makosa na kinyume cha Sheria na Kanuni za Madini kwa mtu mmoja kujilimbikizia eneo kiasi hicho, na makosa mengine ni kuwa yapo maeneo ambayo hajayaendeleza na sheria inaweka bayana kuwa baada ya miaka 2 mtu asiyeendeleza eneo lake anatakiwa kunyang'anywa asilimia 50 ya eneo hilo, na usipoliendeleza lililobaki  katika miaka 2 ijayo unapoteza eneo zima, hivyo kwa maeneo ambayo Mzee Mengi anayamiliki na hajayaendeleza ni vyema sheria ikafuata mkondo wake na anyang'anywe maeneo hayo.


Kauli za Mzee Mengi na mtindo wa Shutuma zake kwa Waziri ulionesha ni kwa kiasi gani Mzee Huyu amekosa busara na hekima katika kufuatilia na kufikisha hoja zake, lakini utumiaji wa vyombo vya habari anavovimiliki na vile ambavyo ana ushawishi navyo kuwashutumu mahasimu wake na hata kuwakatisha tamaa watanzania juu ya mipango na mikakati ya maendeleo ya Serikali yao ni makosa mengine ya msingi katika tasnia ya habari na kwake kama mmiliki, makosa ambayo ni ya kukusudia na yenye kutoa taswira mbaya mbele ya jamii.

Umefika wakati wa watanzania kuwaelewa watu hawa ambao katika macho ya jamii wanajipambanua kama wapigania haki, wakweli na wenye huruma hali ya kuwa uhalisia wa ndani ni watu wabadhirifu, walafi na walanguzi wasiotosheka.

No comments:

Post a Comment