Thursday, January 23, 2014

BALOZI KAGASHEKI AWASILI BUKOBA AAHIDI KULA SAHANI MOJA NA MEYA AMANI ASIYEPENDA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA LA KUMTAKA AACHIE NGAZI

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Bukoba mjini akiratibu mkutano wa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Sued Kagasheki uliofanyika kwenye uwanja wa Bukoba.
Balozi Kagasheki akipongezwa alipofika kwa mara ya kwanza jimboni baada ya kujiuzulu wadhifa wake wa nafasi ya uwaziri wa maliasili na utalii.
Mjumbe wa NEC CCM wa wilaya ya Bukoba, Abdul Kagasheki naye hakubaki nyuma.
Baadhi ya wananchi waliojitoikeza kumpokea.
Balozi Kagasheki akiongea na wananchi wa jimbo la Bukoba mjini, katika hotuba yake amesisitiza kuwa Meya Amani sio Meya kama anavyotangaza kupitia kwenye vyombo vya habari kuwa hakubaliani na taarifa wa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali, anasema kama anasema hajajiuzulu atakumbana na kura za kutokuwa na imani naye, amemtaja Meya Anatory Amani kuwa ni ndiye chanzo cha kudumaza maendeleo katika manispaa ya Bukoba, anasema kiasi cha bilioni zaidi ya 2 ambazo amezitumia bila maelezo kuwa zingefanya shughuli nyingi za kuwaletea maendeleo wananchi.
Baadhi ya viongozi wa CCM walioudhuria mkutano uliandaliwa na Balozi Kagasheki.

No comments:

Post a Comment