Sehemu ya utekelezwaji wa mradi, hili ni eneo ambalo linajengwa tanki la kuhifadhi maji toka kwenye chanzo cha maji cha ziwa Victoria na kuyasambaza kwenye matenki ya Kashura na Ibula, tanki hili limejengwa eneo la Bunena.
Matenki madogo ya kuchuja maji.
Baadhi ya wasimamizi wa mradi wakiwa pamoja na mmiliki wa mtandao huu ambaye ni pia ni mwakilishi wa clouds Tv na Redio Kagera, Audax Mutiganzi wa pili kutoka kushoto, Wa kwanza kushoto ni mhandisi Thomas George meneja wa kampuni inayofanya ukandarasi ya TECHNO FAB toka nchini India, wa pili toka kulia ni Mhandisi Fortunatus Kasimbi ambaye ni mwakilishi wa kampuni inayosimamia mradi huo ya GWK Consult ya nchini Ujerumani.
Mhandisi Kasimbi akielezea jambo wakati akionyesha eneo la chanzo chanzo cha maji cha mradi huo
Mhandisi George akielezea namna maji yatavyochujwa wakati akionyesha chumba ambacho zitafungwa mashine za kuchuja maji.
Huu ndio mtamba utakaoongoza machine zote za kuchunja, kusukuma na kusambaza maji kwenye matenki, mtambo huu ni wa kielekronic pia utatumika kujua habari za matatizo ya kiufundi kwenye mitambo.
Wahandisi, Thomas na Kasimbi wakijadili jambo, walikuwa ndani ya chumba cha mtambo maalumu wa kuendesha mashine.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maji katika mji wa Bukoba (BUWASA) akielezea hali ya upatikanaji wa maji hatika mji huo, anasema kuwa mahitaji ya maji katika mji wa Bukoba ni lita milioni 14 kwa siku wakati uzalishaji wa maji kwa sasa ni lita milioni 8 kwa siku, anasema kuwa mradi huo utasaidia kupunguza mahitaji ya maji katika mji huo.
No comments:
Post a Comment