Ndugu Wanahabari
Uchaguzi Mkuu wenye lengo la kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini.
Uchaguzi Mkuu wenye lengo la kuwapata Madiwani, Wabunge na Rais nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini.
Nimekuwa nikitembelea
vijiji na kata mbalimbali za Wilaya ya Kilombero. Hivi karibuni nilitembelea
kata zote za wilaya, nilizungumza na wananchi, wengi wao walinishauri kugombea
Ubunge. Wananchi wanaamini kuwa kwa pamoja tutaweza kuendeleza vema gurudumu la
maendeleo kwa kasi zaidi.
Wananifahamu kama
mtoto wa masikini mwenzao niliyewahi kuzunguka mitaani kupiga picha ili
kuendesha maisha, mtoto wa masikini niliyewahi kuwa na ofisi ya kusafisha viatu
vya watu eneo la Ubungo Maziwa kwa mzee Mrisho ili niweze kupata nauli ya
kwenda shule wakati huo nasoma Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).
Maisha nayafahamu
vizuri na nina uchungu nayo, natamani kushirikiana na wananchi ili kuepukana na
maisha duni. Katika maisha yangu kutokula au wakati fulani kutembea kwa miguu
kwenda chuo CBE na kurudi nyumbani Ubungo Maziwa (nilikuwa naishi kwa dada),
lilikuwa ni jambo la kawaida, kwani maisha yalikuwa magumu mno.
Sauti ya wananchi wa Kilombero
Kilio cha wananchi pamoja
na mambo mengine ni kwamba wanahitaji kiongozi kijana mwenye nguvu za kuongoza,
kiongozi mwenye ujuzi wa namna ya kuongoza na kutawala, kiongozi ambaye atakuwa
bega kwa bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. Kiongozi
ambaye anajua namna ya kuongoza, siyo namna ya kuhonga au kuwalisha yamini
wapiga kura, kwani wanachohitaji watu wa Kilombero ni maendeleo, siyo zaidi. Hawahitaji
kiongozi ambaye ni maarufu kwa kutembelea magari ya kifahari, wanahitaji huduma
za kijamii kama shule, hospitali na wao wenyewe kusaidiwa namna ya kubuni
miradi ya maendeleo.
Elimu yangu ya juu ni
Stashahada ya Uzamili katika Uongozi na Utawala (Postgraduate Diploma in
Leadership and Governance), kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma-Dar es Salaam
niliyohitimu Aprili 22, 2014. Hata hivyo nje ya elimu nimekuwa nikishughulika
na masuala ya kijamii kupitia kufanya mikutano ya ana kwa ana na jamii katika
masuala ya ujasiriamali, uchumba/ndoa na kadhalika.
Mojawapo sababu za
wananchi kuamini kwamba ninaweza kushirikiana nao kwa ufanisi ni rekodi ambazo
wananchi wenyewe wanazo juu yangu, kwani nimekuwa nao karibu katika mambo mengi
ya maendeleo ikiwamo kushirikiana nao moja kwa moja au vikundi vyao hasa vya walemavu, kina mama, vijana na kadhalika
kama mshauri wao katika suala zima la namna ya kuviendesha na kuwaunganisha na
taasisi au watu wa kusaidiana nao.
Kwa hivi sasa maeneo
kadhaa ya Kilombero yanasaidiwa na mashirika mbalimbali yakiwamo ya nje, baadhi
yake ni kutokana na jitihada zangu….nje ya uandishi wa habari, pia nimekuwa
nikimiliki kampuni ya kuwaunganisha watu na vyuo vya nje ya Global Source Watch
(GSW), ambayo imekuwa ikinipa fursa ya kujuana na watu wengi wa nje.
Nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nitachukua fomu ya kugombea Ubunge kutokana na kukidhi vigezo vyote ya kugombea nafasi hii kama ilivyojieleza katika Katiba ya Tanzania ibara ya 67.-(1) ambayo pamoja na mambo mengine inasema “Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
Nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nitachukua fomu ya kugombea Ubunge kutokana na kukidhi vigezo vyote ya kugombea nafasi hii kama ilivyojieleza katika Katiba ya Tanzania ibara ya 67.-(1) ambayo pamoja na mambo mengine inasema “Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
(a)
ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri
wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili
au Kiingereza;
Mimi ni mzaliwa wa Kijiji cha Mofu, wilaya ya
Kilombero mkoani Morogoro, Juni 26, 1976. Nimewahi kufanya kazi katika vyombo
mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi ikiwamo the Guardian Limited kama
mwandishi wa kujitegemea, Uwazi kama Mhariri, Leo ni Leo kama Mhariri wa
Makala, Mwananchi kama Mwandishi wa makala baadaye mhariri wa jarida la ndani
ya biashara, the Media Project (Marekani) kama mchangiaji nk.
Kwa sasa ni Kiongozi wa Utafiti hapa nchini
(National Lead Researcher) wa taasisi ya kimataifa iitwayo Global Integrity
yenye makazi yake Marekani, pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwanahabari,
lakini maamuzi haya ya kugombea ubunge ni yangu binafsi hayana uhusiano wala
hayataingiliana na sehemu yoyote ninayofanyia kazi.
Nimewahi kutembea katika nchi mbalimbali kwa
lengo la kwa kusoma na kutembea, baadhi yake ni Marekani, Kenya, Uganda, Dubai,
Thailand, India.
OMBI
KWA WASAMARIA WEMA
Napenda kuchukua fursa hii pia kuwaomba
wasamaria wema kuangalia namna ya kusaidiana na wananchi wa Kilombero kwani wakati
huu njia nyingi hazipitiki kwa sababu barabara zimejaa maji kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha. Magari yamekuwa hayapitiki katika maeneo mengi ya
Kilombero kwa sasa.
Kwa mfano sehemu kubwa ya barabara ya
kutoka Ifakara kwenda Mofu haipitiki,
kiasi kwamba wagonjwa wamekuwa hawawezi kubebwa kupelekwa Ifakara ambako ndiko
pekee kuna hospitali ya Wilaya, St Francis. Wapo baadhi ya wagonjwa wamekuwa
wakibebwa kwa kutumia baiskeli na hata pikipiki, jambo ambalo limekuwa gumu
hasa kwa wajawazito.
Magari ya abiriia hasa Noah zilizokuwa
zikifanya safari kutoka na kuingia Ifakara kutoka vijiji mbalimbali vya Wilaya
ya Kilombero yamesitisha safari kutokana na barabara kujaa maji. Yapo magari
machache hasa ya mizigo ambayo nayo yanafika baadhi ya vijijini kwa shida
yakiwa yamebeba mizigo na abiria hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi.
Mvua zimeathiri pia kilimo, kwani mashamba
mengi yamefurika maji, huku kukiwa na njaa kwa baadhi ya wanavijiji. Hivyo
nachukua fursa hii kuiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kusaidia wananchi
wakiwamo wa vijiji vya Mofu, Ihenga, Mlimba, Chisano, Chita, Mkula, Sanje, Uchindile na Utengule
Imetolewa leo tarehe
12, Mei 2015,
na Dismas Lyassa
(Mtangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM)
0754 49 8972/0712183282
(Mtangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM)
0754 49 8972/0712183282
No comments:
Post a Comment