Jumuiya ya Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mjumbe wa tume ya
mabadiliko ya katiba Dr Sedondo Mvungi ambacho kimetokea katika hospitali ya
Millpark nchini Afrika kusini.
Uongozi wa UVCCM
Taifa unatoa pole kwa familia na ndugu wa marehemu, pia UVCCM inatoa pole kwa
uongozi wa NCCR- Mageuzi na kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji
Warioba pamoja na Vijana nchini kote ambao wamenufaika na Utaalamu na mafunzo.
Kama vijana tulihitaji sana mchango wa mawazo, hekima na utaalamu kutoka kwake,
hakika tumepoteza kiongozi shupavu, muadilifu na mzalendo ambae ni mfano wa
kuigwa kwa Vijana wa Taifa hili.
Kadhalika, UVCCM
inatoa pongezi za dhati kwa hotuba makini iliyojaa hekima, busara na ushupavu
wa Uongozi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Hakika vijana tumeridhishwa na maamuzi ya
Mheshimiwa Rais ya Kuendelea kuwa Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) na tunapongeza maamuzi hayo yanayolenga kudumisha Umoja na Ushirikiano wa
Nchi za kiafrika katika kujiletea maendeleo. Kwa kutambua nafasi na manufaa
yanayopatikana kwa vijana kutokana na fursa za kiuchumi, kisiasa, kijamii,
ajira nk UVCCM Inamuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa uamuzi wake huo.
Pamoja na kuunga
mkono uamuzi huo, UVCCM inatoa angalizo kuwa ni vyema kwa nchi zote wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuendelea kuheshimu taratibu na kanuni za
jumuiya hiyo ili kuifanya endelevu, imara na mfano kwa nchi nyingine za Afrika
na Duniani kwa ujumla. Ni lazima wazingatie kuwa Umoja na Mshikamano ndio nguzo
ya maendeleo ya kweli ya Afrika.
Pia, Umoja wa Vijana
wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesikitishwa na tuhuma ambazo zimeripotiwa
kwenye vyombo mbalimbali vya habari kutoka kwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA)
Mheshimiwa Godbless Lema ambazo amezielekeza kwa baadhi ya Viongozi wa Jumuiya
akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM Ndugu Sadifah Juma kuwa amehusika na
usambazaji wa Picha chafu mitandaoni.
Pamoja na
kusikitishwa, UVCCM inazo taarifa juu ya mgogoro unaoendelea katika Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kwamba inamtaka Lema kutoelekeza tuhuma
kwa UVCCM na viongozi wake bali waangalie namna bora ya kushughulikia na
kutatua migogoro yao ya ndani ambayo imesababisha kuzushiana, kuchafuana na
kuvujishiana siri katika mitandao hasa ya kijamii.
UVCCM na Viongozi
wake inakana kwa namna yeyote ile kuhusika na usambazaji huo na kwamba Jumuiya
hii ni ya Vijana makini na wanaojitambua na inajielekeza katika kufanikisha
malengo ya kuundwa kwake ya kukisaidia Chama kushika dola mwaka 2015.
Na kwamba UVCCM
inalaani tabia ambayo imeasisiwa na Vijana wa CHADEMA ya kukashifu, kuzomea na
hata kutukana Viongozi wa CCM na Serikali yake na kwamba yaliyomkuta Mhe Lema
ni matunda ya kazi waliyoiasisi wenyewe.
Imetolewa na:
PAUL
MAKONDA
KATIBU
WA IDARA YA HAMASA NA CHIPUKIZI
UVCCM
13/11/2013
No comments:
Post a Comment