ALLY OMARY CHITANDA
MWENYEKITI WA CHADEMA
MKOA WA LINDI
30/11/2013
KATIBU WA CHADEMA
MKOA WA LINDI
YAH; KUJIUZURU UENYEKITI WA MKOA
Somo la hapo juu
lahusika.
Napenda kuchukua nafasi
hii kukuarifu kuwa kwa hiari yangu bila ya kushawishiwa na mtu yeyote, nimeamua
kujiuzuru nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa tangu leo tarehe 30/11/2013.
Nashukuru sana kwa
ushirikiano wako pamoja na Vionmgozi wote wa Baraza la Uongozi pamoja na Baraza
la Mashauriano la Mkoa, lakini pia niwashukuru Viongozi wote wa Majimbo naWilaya
hasa Nachingwea ambao kwa kiasi kikubwa, wameniwezesha kufika hapa hasa wakati
mgumu wa Ujenzi wa Chama na kugombea Ubunge 2005 na 2010.Matarajio yangu
ya kuweza kukomboa wanyonge kupitia CHADEMA kwa sasa sioni kama yanaweza kufikika.
Nitabaki kuwa Mwanachama
wa kawaida na ninaahidi kuwa Mwanachama
mwaminifu na pale nitakapohitajika nikotayari
kusaidiana na Viongozi kujenga
Chama.Nawataki kazi njema na Ujenzi wa Chama.
Ahsante kwa ushirikiano.
………………………………..
A.O. CHITANDA
No comments:
Post a Comment