Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
nchini Tanzania mwishoni mwa wiki kilitunuku digrii ya Heshima Mwana
fasihi na mwandishi wa vitabu maarufu Afrika Profesa Ngugi wa Thiong'o.
Ngugi alitunikiwa digrii ya Uzamivu wa Fasihi
"Doctor of Literature" ambayo ni ya pili kutunikiwa barani Afrika baada
ya aliyotunikiwa kutoka Chuo Kikuu cha Walter Sesulu cha Afrika ya
Kusini.Akizungumzia kuhusu heshima hiyo aliyopewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ngugi amesema amefurahishwa kwa kuwa Chuo hicho kikuu kimetambua mchango wake katika fani ya fasihi na uandishi wa vitabu.
Akizungumzia kuhusu waandishi vijana wanaochipukia Ngugi amesema amefurahishwa kuona na baadhi ya waandishi vijana ambao wanafuata nyayo zao kwa kuandika mambo yanayogusa jamii na kuibua mambo mazito.
Kuhusu maono ya kuandika kitabu kitakachohusu matukio yaliyotokea Kenya hivi karibuni Ngugi amesema anatafakari na upo uwezekano akaandika kitabu kinachohusu hayo yaliyotokea.
No comments:
Post a Comment