Tume ya Mabadiliko ya Katiba
nchini Tanzania imepata pigo baada ya mmoja wa wajumbe wake Dr. Sengondo
Mvungi kufariki dunia nchini Afrika Kusini, ambako alikuwa akitibiwa.
Dr. Mvungi, alipelekwa Afrika Kusini kwa
matibabu zaidi baada ya kuvamiwa na watu wanaoaminika kuwa majambazi
nyumbani kwake mjini Dar, es Salaam, wiki iliyopita."Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo Jumanne, Novemba 12, 2013 saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini," amesema Bwana Rashid katika taarifa yake fupi.
No comments:
Post a Comment