Monday, October 15, 2012

MKUU WA MKOA KAGERA APIGA MARUFUKU MIADHARA YA DINI



MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe amepiga marufuku miadhara  ya inayoendeshwa  mkoani na humo inayofanyika kwa lengo la kukashfu madhehebu mengine ya dini.

Massawe ametoa tamko hilo hivi karibuni wakati wa kikao cha ushauri cha mkoa wa Kagera kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wake katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba.

Akiongea alisema miadhara ya dini inayoendeshwa kwa lengo la kukasifu madhehebu mengine inachafua hali ya hewa kwa kuwa ndio kwa kiasi kikubwa inachangia uvunjifu wa amani ndani ya jamii.

“Nimesikia miadhara ya dini inayokashfu madhehebu mengine inaendeshwa kwenye maeneo ya Kyaka na Katoro, viongozi wenzangu nawaagiza kawakamata mtu yoyote mtakayemuona anaaendesha muadhara wa kulikashfu dhehebu jingine” Alisema.

Massawe alisema wanaoendesha miadhara  inayokashfu madhehebu mengine ni waharifu kama waarifu wengine, “Sheria za nchi yetu zinasema kila mtu anao uhuru wa kuabudu kila kuingiliwa na mtu yoyote, nasema anayeingilia imani ya mtu mwingine niu msaliti, Traiter” Alisema msisitizo.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka waumini wa madhehebu ya dini na viongozi waokupendana, kuheshimiana na kuthaminiana, alisema wakifanya hivyo watakudumisha amani miongoni mwa jamii na pia waimarisha ustawi.

Alisema haina maana waumini wa madhehebu ya dini kuchukiana  kwa kuwa mungu wanayemuanini na kumtafuta ni mmoja  labda njia ya kumfikia ndio inatofautiana , “ninachokijua kila mtu anayo namna ya kumfikia mungu, hivyo kila njia inayotumiwa na mtu kumtafuta mungu ni lazima ieshimiwe” alimaliza.

No comments:

Post a Comment