Huyu ndiye mbunge wa jimbo la Nkenge Asumpta Mshama.
MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe amepinga
vikali ushauri uliotolewa mbunge wa jimbo
la Nkenge Asumpta Mshama wa kuiomba
serikali iwaruhusu wakulima wao wenyewe wajitafitie masoko wa kahawa
wanayoizalisha ndani na nje ya nchi.
Massawe amesema kamwe biashara ya kahawa haitakuwa huria
hivyo wakulima wataendelea na utaratibu uliowekwa na serikali wa kuuza kahawa
yao kwenye vyama vya ushirika na makampuni ya yaliyosajiliwa kisheria
yanayofanya kazi ya kununua kahawa toka kwao.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha
kamati ya ushauri ya mkoa wa Kagera kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa mkuu
wa mkoa uliko kwenye manispaa ya Bukoba.
Alisema kuwa wakulima wanapouza kahawa kwa njia isiyo rasmi
wanakuwa wanaikosesha serikali mapato , “halmashauri za wilaya na manispaa huwa
zinanufaika na mauzo ya kahawa kwa kupata ushuru tukiruhusu biashara huria ya
kahawa tutakuwa tuaziua halmashauri za wilaya na manispaa” alisema Massawe.
“Sikubaliani na kauli ya mhemimiwa mbunge biashara ya kahawa
kamwe haitakuwa huria, na mimi naahidi titaendelea kuwashughulikia kikamilifu
wale wote wanajihusisha biashara ya magendo ya kahawa, ni lazima tuunusuru
uchumi wetu” alisema huku akishangiliwa.
Massawe alisema kamwe hatamfumbia macho mtu yoyote atakayejihusha
na magendo ya kahawa’ “Nitamshughulikia mtu yoyote bila kuangalia sura yake,
kabila na nafasi yake aliyonayo ndani ya jamii” alisema.
Aliwataka viongozi wote washirikiane ili wawezer kuwathibiti
wale wote wanajihusisha na magendo ya kahawa, alisema magendo ya kahawa
inavidhoofisha vyama vya ushirika na wakulima wanaouza kahawa yao kwa njia ya
magendo, “wakulima wanaouza kahawa kwa njia ya magendo wanapunjwa sana” alimaliza
kusema.
No comments:
Post a Comment