JESHI la polisi mkoani Kagera limeanza kutekeleza mkakati
wake mpya ambao limeubuni wa kuwahamasisha wananchi mkoani humo kupima afya zao.
Mkakati huo ulidhihirika mwishoni mwa wiki baada jeshi
hilo kuendesha zoezi la kuwapima wananchi wa manispaa ya Bukoba na maeneo
mengine virusi vinavyoambukiza ugonjwa wa UKIMWI.
Katika zoezi hilo lililofanyika kwenye maeneo ya standi kuu
ya mabasi zaidi ya wananchi zaidi 1,500 walijitokeza kupima virusi vya UKIMWI
kwa hiari.
Akiongea wakati wa zoezi hilo la upimaji mrakibu msaidizi wa
jeshi la polisi Dr Hussein Gamu ambayo aliendesha zoezi hilo kwa kushirikiana
na maofisa wengine wa jeshi hilo alisema mkakati wa jeshi hilo wa kuanzisha
utaratibu wa kupima wananchi afya zao unalinga kuimarisha mahusiano kati ya
jeshi hilo na wananchi.
Gamu alisema jeshi la polisi lina mkakati mkikati ya kuimarisha ustawi wa wananchi, alisema
wananchi wanapokuwa na ustawi wanakuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu
yao vizuri.
Afisa huyo alisema kuwa wananchi ndio nguzo kubwa ya jeshi la polisi, aliendelea kusema wananchi
ndio wanalipa nguvu jeshi hilo liweze kutekeleza majukumu yake vizuri.
Alisema taarifa zinazotolewa na wananchi zinazohusiana na
masuala ya uharifu kuwa ndizo zinazolisaidia
jeshi la polisi kukabiliana na matukio ya uharifu kwa kiasi kikubwa.
Gamu alisema jeshi hilo litaendelea kuwa karibu na wananchi
hasa kupitia kwenye dhana yake maalumu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi,
alimaliza kwa kuwaomba wananchi waendelee kulipa ushirikiano jeshi hilo ili
waweze kunufaika nalo zaidi.
No comments:
Post a Comment