Tuesday, October 30, 2012

MSIMU WA KITUWEO CHA HESHIMA 'SENENE' WAANZA KAGERA

 Baadhi ya wakazi wa mji wa Bukoba wakichangamkia senene.
 Wanafunzi hawakubaki nyuma, huyu ni mmoja wa wanafunzi waliochangamkia senene wajianza kuonekana mkoani Kagera.
 Kitoweo hicho kikiwa sokoni.
 Senene wakirandaranda juu ya magunia.

Wafanyabiashara ya senene wakifanya vitu vyao.

Monday, October 29, 2012

RAIS KIKWETE ATUA KILIMANJARO


Picha na Ikulu.

MKE WA WAZIRI PINDA ATUNUKIWA SHAHADA

  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipokea  zawadi ya ua kutoka wadogo zake Salma Rehani (kulia), Mkaroga Rehani (wapili kulia) na Mabe Rehani baada ya kutunukiwa Shahada ya Uongozi wa Biashara  katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, John Samwel Malecela akimtunuku Shahada ya Uongozi wa  Biashara, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria  yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho Kibaha Oktoba 27, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Sunday, October 28, 2012

MAMBO YA IDD HAYO

 Familia ya afisa wa jeshi la polisi, Zuberi.
Familia ya mhamdisi Kijigo.

WADAU WA HARUSI YA NJUNWA

Kutoka kushoto ni Edward Jothwan na anayefuata ni Bwana harusi mtarajiwa Edius Njunwa.

Saturday, October 27, 2012

KIKAO CHA MAANDALIZI YA HARUSI YA EDIUS NJUNWA

Viongozi wa kamati ya maandalizi ya harusi ya Edius Njunwa Mwesiga kilichofanyika kwenye viwanja vya Jimkana.
Wajumbe wa kikao cha maandalizi ya harusi.

Friday, October 26, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAZI KWA MAWAZIRI NA MAAFISA WAANDAMIZI WA SERIKALI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha kazi (retreat)  cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali wanaokutana kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Pamoja naye meza kuu ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali (kulia) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

MKUU WA MKOA KAGERA ATOA ZAWADI YA IDD

 Sehemu ya zawadi iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe kwa vikundi visivyojiweza kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Idd, hawa ni mbuzi.
Massawe akitoa zawadi kwa msimamizi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Uyacho kilichoko Hamgembe, Kagera.
 Msimamizi wa kituo cha kulelea yatima cha Nusuru yatima akipokea zawadi ya sikukuu ya Idd.
 Massawe akimungalia mmoja wa yatima wanaolelewa katika kituo cha Nusuru yatima kilichoko Kashai, alichukizwa na hali aliyokuwa nayo mtoto huyo.
 Msimamizi wa kituo cha kulea wazee cha Kiilima akipokea zawadi ya mbuzi toka kwa Massawe.
Baadhi ya viongozi mkoani Kagera walioudhuria tafrija fupi ya kukabiddhi zawadi ya Idd kwa wasiojiweza, ilifanyika kwenye viwanja vya Ikulu ndogo iliyoko katika manispaa ya Bukoba.

Wednesday, October 24, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA NANE WA UVCCM MJINI DODOMA

Bendi ya muziki ya Vijana Jazz Orchestra 'Wana Pambamoto' ikitumbuiza kwa wimbo maalumu katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma ikiwa ni shamra ya kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi toka kwa  Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa UVCCM Bw. Benno Malisa katika  ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012

Tuesday, October 23, 2012

MNYAUKO BACTERIA WATISHIA USALAMA WA NDIZI KAGERA

UGONJWA unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria umeanza kuathiri upatikanaji wa ndizi kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera.

Ugonjwa huo unasambaa kwa kasi hasa kwenye maeneo ya wilaya za Muleba na Karagwe ambayo uzalisha  ndizi nyingi mkoani Kagera na maeneo mengine ya wilaya za Bukoba na Misenyi.

Hali ya ugonjwa huo unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria imechangbia kupunguza uzalishaji wa ndizi mkoani Kagera jambo ambalo limechangia kupanda kwa bei ya ndizi zinapopelekwa kwenye masoko.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba kwenye soko kuu la Bukoba ndizi kubwa inauzwa kwa wastani wa kati shilingi 15,000 hadi 20,000 ambapo miaka iliyopita ndizi kubwa zilikuwa zinauzwa kwa wastani wa kati ya shilingi 6,000 hadi 8,000.

Kupanda kwa bei ya ndizi iliyochangiwa na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa migomba kumewalazimisha baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera ambao hutegemea ndizi kama chakula chao kikuu kubadilika ambapo sasa wanalazimika kula ugali na wali.

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera wamelazimika kubadili fikira zao za kudhani kuwa ndizi ndicho chakula kikuu baada ya kushindwa kumudu gharama za kununua ndizi kwenye masoko ambazo bei yake ni kubwa.

Baadhi ya wakulima bora wa migomba mkoani Kagera ambao mashamba yao yameathirika kutokana na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa mogomba ni pamoja kamishina mstaafu wa jeshi la polisi Alfred Tibaigana.

Kamishina Tibaigana shamba lake liko katika kijiji cha Buganguzi wilayani Muleba limeathirika sana, Mkulima huyu kabla ya ugonjwa huu alikuwa na uwezo wa kuzalisha wastani tani 40 za ndizi kwa wiki ambapo sasa anazalisha wastani wa tani zisizozidi 10 kwa wiki.

Aidha, baadhi ya wakulima mkoani Kagera wameitahadharisha serikali kuchukua hatua za haraka za kuthibiti ugonjwa huu unaosambaa kwa kasi ili zao la ndizi mkoani Kagera lisibaki kwenye vitabu vya historia.

Monday, October 22, 2012

RAIS KIKWETE KATIKA KILELE CHA MKUTANO MKUU WA UWT DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT.

YAJUE MAENEO YA MANAYOPAMBA MJI WA BUKOBA

 Barabara ya Kashozi iliyoko katika manispaa ya Bukoba.
 Barabara ya kuelekea tarafa ya Bugabo.
 Standi kuu ya mabasi yaendayo Bugabo iliyoko katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba.
 Mitaa ya manispaa ya Bukoba.
 Mandhari ya mzunguko uliko karibu na standi kuu ya mabasi.
 Eneo la standi kuu ya mabasi.
 Sanamu ya mgomba iliyoko kwenye mzunguko mkuu wa manispaa ya Bukoba.
Mandhari ya maeneo ya uswahilini.

Sunday, October 21, 2012

JESHI LA POLISI KAGERA LINAVYOFANYA KAZI YA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUPIMA AFYA ZAO

JESHI la polisi mkoani Kagera limeanza kutekeleza mkakati wake  mpya ambao limeubuni  wa kuwahamasisha wananchi  mkoani humo kupima afya zao.

Mkakati  huo  ulidhihirika mwishoni mwa wiki baada jeshi hilo kuendesha zoezi la kuwapima wananchi wa manispaa ya Bukoba na maeneo mengine virusi vinavyoambukiza ugonjwa wa UKIMWI.

Katika zoezi hilo lililofanyika kwenye maeneo ya standi kuu ya mabasi zaidi ya wananchi zaidi 1,500 walijitokeza kupima virusi vya UKIMWI kwa hiari.

Akiongea wakati wa zoezi hilo la upimaji mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi Dr Hussein Gamu ambayo aliendesha zoezi hilo kwa kushirikiana na maofisa wengine wa jeshi hilo alisema mkakati wa jeshi hilo wa kuanzisha utaratibu wa kupima wananchi afya zao unalinga kuimarisha mahusiano kati ya jeshi hilo na wananchi.

Gamu alisema jeshi la polisi lina mkakati mkikati  ya kuimarisha ustawi wa wananchi, alisema wananchi wanapokuwa na ustawi wanakuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu yao vizuri.

Afisa huyo alisema kuwa wananchi ndio nguzo kubwa ya  jeshi la polisi, aliendelea kusema wananchi ndio wanalipa nguvu jeshi hilo liweze kutekeleza majukumu yake vizuri.

Alisema taarifa zinazotolewa na wananchi zinazohusiana na masuala ya uharifu kuwa  ndizo zinazolisaidia jeshi la polisi kukabiliana na matukio ya uharifu kwa kiasi kikubwa.

Gamu alisema jeshi hilo litaendelea kuwa karibu na wananchi hasa kupitia kwenye dhana yake maalumu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi, alimaliza kwa kuwaomba wananchi waendelee kulipa ushirikiano jeshi hilo ili waweze kunufaika nalo zaidi.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KENYA IKULU DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa  Jakaya Mrisho Kikwete ametaka wananchi wa Kenya wapewe nafasi ya kuamua ni viongozi gani wanawataka katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Machi mwakani.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kenya wanayo haki ya msingi kabisa kuamua hatma ya taifa lao katika Uchaguzi Mkuu huo.

Mheshimiwa Rais aliyasema hayo leo Oktoba 21, 2012 alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya nchini Kenya uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam.

Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. Wote wawili ni wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao.
Wengine katika msafara huo walikuwa ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu, Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli.

Rais Kikwete aliwapongeza kwa kuamua kufanya kazi kwa pamoja licha ya kuwa watakuwa  washindani katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu huo.

Mheshimiwa Rais ameitakia heri nchi ya Kenya katika uchaguzi huo ujao, na kusisitiza kwamba nchi hiyo ya jirani ina umuhimu katika mustakabali wa kiuchumi kwa nchi  za Afrika Mashariki.

Rais Kikwete wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alikuwa miongoni mwa viongozi walioshughulika sana kutafuta ufumbuzi wa ghasia na vurugu zilizozuka kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Rais Kikwete alikaa siku tatu nchini Kenya akitafuta usuluhishi wa vurugu hiyo ya kisiasa nchini humo, ambayo katika mazungumzo yake leo ameyataja kama ajali iliyolipata Taifa la Kenya, na ambayo majirani wake hawaitarajii kutokea katika uchaguzi ujao.
Mwisho

Imetolewa na:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
DAR ES SALAAM,
21 Oktoba, 2012

Friday, October 19, 2012

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.

MKUTANO WA KUJADILI SEKTA YA GESI ASILIA

  Meneja wa Sekta Kupunguza Umaskini na Kusimamia Maendeleo ukanda wa Afrika wa Benki ya Dunia Dkt Albert Zeufack, akongea wakati wa mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini, akiwa ameongozana na mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na Timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na  inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya waandishi wa habari baada ya mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini.Mkutano huo ulihudhruiwa pia na  mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na  inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani ilipotembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Bw. Mathias Chikawe, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzan Mlawi na maafisa waandamizi  wa Ofisi ya Rais, kamati hiyo


PICHA NA IKULU

KAMATI YA BUNGE INAYOSHUGHUKIA UUNDWAJI WA SHERIA NDOGO NDOGO YAMALIZA KAZI YAKE KAGERA

Mkuu wa mkoa wa kagera kanali mstaafu Fabian Massawe akipongezana na mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoghulikia sheria ndodo ndogo baada ya kikao cha majumuisho za ziara ya kamati hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kagera.
Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Muleba, Richard Katomero (kushoto).
Massawe akiongea na watendaji wa halmashauri za wilaya na manispaa.

Thursday, October 18, 2012

KAMATI YA BUNGE INAYOSHUGHULIKIA MASUALA YA TUNGAJI WA SHERIA NDOGO NDOGO

 Wabunge wanaounda kamati ya bunge inayoshughulikia sheria uundwaji wa sheria ndodo ndogo
 Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabian Massawe akiongea na kamati ya bunge ofisini.