Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
ameunda uchunguzi wa nje kuhusu kashfa ya kuwadhalilisha watoto
kulikofanywa na wanajeshi wa Ufaransa wa kulinda amani nchini Jamahuri
ya Afrika ya Kati.
Kuundwa kwa kamati huru ya uchunguzi ni moja ya madai ya wakosoaji ambao wamekuwa wakiukosoa Umoja wa Mataifa kwa kutochukua hatua madhubuti kuchunguza madai hayo ya udhalilishaji watoto wengine wakiwa na miaka tisa.Hatua hii imekuja mwaka mmoja kamili baada ya watafiti wa Umoja wa Mataifa kusikia kwanza kutoka kwa watoto walioathirika kutokana na udhalilishaji huo katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika Kati, Bangui.
No comments:
Post a Comment