Takriban mbwa 10,000 watachinjwa na nyama yao kuliwa katika sherehe hizo
zitakazofanyika katika eneo la Yulin mkoa wa Guangxi siku ya jumapili
na jumatatu ili kuadhimisha kuanza kwa msimu wa joto kulingana na vyombo
vya habari vya kitaifa.
Mwalimu mmoja aliyestaafu kutoka Tianjin aligonga vyombo vya habari alipowanunua mbwa wengi ili kuwanusuru
Wakaazi na wafanyibiashara huko Yulin wanasema kuwa wanyama hao huuawa kwa njia nzuri.
Wanaharakati wanasema kuwa mauaji hayo ni ya kikatili na kwamba kampeni
ya mitandaoni ya kupiga marufuku sherehe hiyo imetiwa sahihi na zaidi ya
watu milioni 3.8 kufikia sasa na kampeni hiyo kuungwa mkono na watu
wengi mwaka huu kutoka watu maarufu wa kitaifa na kimataifa.
Watu maarufu akiwemo mcheshi wa Uingereza Ricky Gervais wamezungumza katika mtandao wa Twitter na alama ya reli StopYuLin2015.
Nyota wa muziki nchini Uchina Chen Kun na msanii Yang Mi wamesema kuwa wanaiunga mkono kampeni hiyo katika mtandao wa Weibo.
No comments:
Post a Comment