Wizara ya Sheria ya Marekani
imechapisha taarifa inayoelezea jinsi Afisa wa zamani wa FIFA Chuck
Blazer alivyokiri kuwa yeye pamoja na wenzake walipokea rushwa ikiwa ni
pamoja kuichagua Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa fainali ya kombe la
dunia mwaka 2010.
Taarifa hiyo ambayo inamwelezea Afisa humo wa zamani wa Fifa Chuck Blazer kukiri kupokea rushwa sasa huenda ikaibua mengi kwenye kashfa ya rushwa inayoindamana shirikisho la FIFA.
Mmerakani huyo kwenye taarifa hiyo inadai alikuwa ni mmoja wa watu waliosuka mipango ya kupokea rushwa katika tukio jingine la fainali la kombe la dunia 1998.
Taarifa za Kukiri zipo katika maandishi wakati wa kesi yake mwaka 2013 wakati kesi yake ilipokuwa akisikilizwa katika mahakama ya Easten New York huko Marekani ambapo alikiri makosa kumi yaliyokuwa yanamkabili.
Marekani imefungua kesi ya rushwa inayowakabili maafisa wa FIFA jambo lililofanya Rais wa FIFA Sepp Blatter kuamua kutangaza kujiuzulu.
Mwendesha mashtaka wa Marekani wiki iliyopita aliwashtaki maafisa 14 wa ngazi wa juu wa FIFA tuhuma za rushwa, kutakatisha fedha.
No comments:
Post a Comment