Uongozi wa gazeti la Tanzania daima umepewa
majuma mawili kuwaomba radhi wananchi wa vijiji vya Kiga na Buhanga vilivyoko
wilayani Muleba kwa kukanusha taarifa lilizozichapishwa na gazeti hilo juma lililopita wanazodai kuwa zililenga kuwadhalilisha, kuwachonganisha na kuwagawa wananchi na viongozi wao.
Viongozi waliotoa kauli hiyo ni pamoja na Masoud
Ibrahim ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kiga na Dominic Domician
mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Buhanga kwa niaba ya wananchi ambao walisema
ikiwa uongozi wa gazeti hilo hautawaomba radhi
wananchi wa vijiji hivyo katika
kipindi hicho watafikia uamzi wa kulifikisha mahakamani.
Wakiongea na gazeti hili jana walisema gazeti
hilo liliwadhalilisha wananchi kwa kuchapisha taarifa iliyokuwa inadai kuwa wananchi
wa vijiji hivyo walioungwa pilau na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya
makazi, Profesa Anna Tibaijuka alipofanya mikutano ya hadhara kwa nyakati
tofauti katika vijiji hivyo hivi karibuni.
Walisema taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye
ukurasa wa mbele wa gazeti la Tanzania Daima kuwa ilikuwa sio ya ukweli bali ilikuwa
ni ya uzushi kwa kuwa pilau iliyoliwa na
wananchi wakati Profesa Tibaijuka ambaye
pia ni mbunge wa jimbo la Muleba Kusini alipotembelea vijiji hivyo ilikuwa
imeandaliwa na wananchi wenyewe kuwa wala yeye hakuusika.
“Profesa Tibaijuka alipofika kwenye kijiji changu
cha Buhanga alikuja kuhamasisha
maendeleo na mgeni yoyote akikutembelea ni lazima mkaribishe sisi wahaya
tunasema ‘akamwani’ mimi nashangaa makaribisho tuliyomfanyia waziri watu
kuyatafsiri vingine, hakuandaa pilau bali pilau tuliiandaa sisi viongozi na
wananchi” alisema Dominic kwa masikitiko.
“Nini ninachoshukuru alipofika katika kijii
Buhanga aliazimia kujenga vyumba vinne vya madarasa katika shule ya msingi ya Rulanda, shule ilikuwa
katika hali mbaya wanafunzi walikuwa wakitumia vyumba vya madarasa
vilivyojengwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi, ninachosema ziara yake katika
kijiji change ilikuwa na mafanikio nashangaa wanaombeza” alisema Dominic.
Masouud Ibrahim, mwenyekiti wa serikali ya kijiji
cha Kiga alisema kunapowachafua viongozi tuwakatisha tama hata mambo mazuri
wanayokuwa wameyapanga kuwafanyia wananchi wanalazimika kuyasitisha, aliviomba
vyombo mbalimbali vya habari viandike mambo mazuri wanayoyafanya viongozi badala ya kuandika habari
zinazolenga kuwakatisha tama viongozi hasa wanaofanya harakati kubwa za kuwaletea
wananchi maendeleo.
Alisema kuwa Profesa Tibaijuka ni mhamasishaji
namba moja wa masuala ya maendeleo, aliendelea kusema wanaomsema vibaya
wanalenga kumkatisha tama, aliwaomba wananchi katika jimbo la Muleba Kusini
kupuuza propaganda mbalimbali zinazolenga kumchafua Profesa TIbaijuka.
Masoud aliwaomba wananchi kumuunga mkono kila
jambo linalobuniwa na Profesa TIbaijuka lenye lengo la kuwaletea maendeleo,
alisema kuwa watu ambao kawaida yao ni kupinga kila lililozuri ambao linaweza
kuleta ustawi ndani ya jamii.
Viongozi hao waliwaomba pia wananchi katika
vijiji hivyo kuwa na mshikamano ili waweze kudumisha amani na upendo ndani ya
jamii.
No comments:
Post a Comment