MJUMBE
wa baraza la ardhi la kata Kasambya katika
wilaya ya Misenyi Egidius Medard amehukumiwa na mahakama kwenda jela
kutumia kifungo cha miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi 500,000
baada ya mahakama huyo kuthibitisha tuhuma
zilizokuwa zinamkabili.
Hukumu
hiyo imetolewa hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Bukoba, Sylivia
Lushasi jana baada ya mahakama hiyo kuridhika na ushahidi uliotolewa na
upande na mlalamikaji ulioongozwa taasisi ya kupambana na rushwa
(TAKUKURU) mkoani Kagera.
Mheshimiwa Lushasi alisema mahakama imetoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata wanaotoa hukumu kwa upendeleo kwa ushawishi wa fedha na mali nyingine.
Amesema vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wajumbe wa mabaraza ya ardhi vya kuomba rushwa ili vipindishe hukumu kuwa kamwe havitavumiliwa, hakimu huyo amesema vinawanyima haki baadhi ya watu wamaostahili kupata zao.
Mheshimiwa Lushasi amemaliza kwa kusema hata vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi vinavyojitokeza ndani ya jamii kwa kiasi fulani vinachangiwa na baadhi ya waliopewa mamlaka ya kusimamia amani ambao wanafanya kazi kinyume na taratibu zinazowaongoza.
Mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Fortunatus Mpangamila, awali alisema kuwa Medard alikamatwa na maofisa wa taasisi hiyo julai 5, 2011 akiwa kwenye harakati za kupokea kiasi cha shilingi 200,000, alisema maofisa hao walimnasa Medard baada ya kumuwekea mtego.
Hata hivyo Medard alipelekwa gerezani baada kukosa faini ya shilingi 500, 000 ambayo alipaswa kuitoa kama adhabu hivyo atatumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani.
No comments:
Post a Comment