Kupitia
serikali ya Ujerumani mkoa wa Kagera umepata mtaalam mshauri ambaye anatoa
utaalam wa kuusaidia mkoa katika nyanja mbalimbali za kuinua uchumi wake kwa
kutoa ushauri jinsi ya kutumia fursa zilizopo mkoani Kagera kwa ajili ya kuleta
maendeleo ya haraka kwenye jamii.
Bw.
Joern Bernhadt ni mtaalam aliyebobea katika
kutoa ushauri wa huduma za jamii kwa
miaka 41 kutoka nchini Ujerumani na amewahi kufanya kazi katika nchi mablimbali
kama Indonesia, Swaziland, na Ethiopia.
Bw.
Bernhadt alikutana na Mkuu wa Mkao wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe
pamoja na Wataalam kutoka katika ofisi yake na kutoa ushauri wake juu ya
kongeza ajira katika mkoa wa kagera pamoja na kuendeleza watu wa ngazi ya chini
kielimu kupitia vyuo vya ufundi.
Katika
kutengeneza ajira Bw. Bernhadt alipendekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa
zinaweza kuamua kujenga barabara za mawe ambazo kwa kiwango kikubwa
zinatengeneza ajira kwa watu wengi na kudumu kwa muda mrefu alitolea mfano wan
chi ya Ethiopia ilivyopunguza tatizo la ajira kwa njia hiyo.
“Katika
kutengeneza barabara hizo wananchi watafundishwa jinsi ya kuchonga mawe na
baada ya mawe hayo kuchongwa yatanunuliwa na serikali ili itengeneze barabara
na kwa kufanya hivyo tayari wananchi ambao hawana ajira wanaweza kujiajili
kupitia miradi kama hiyo”. Alishauri Bw. Bernhadt.
Elimu,
Mtaalam huyo aliashauri vyuo vya ufundi kujengwa vingi iwezekanavyo ili
wananchi wengi wapate ujuzi wa ufundi. Lakini alitaadharisha kuwa katika vyuo
hivyo soko ndilo litaje ni huduma gani inahitajika ili walimu watoe elimu
sahihi ya kukidhi soko husika na siyo kufundisha ufundi tu.
Uchumi,
katika kukuza uchumi wa mkoa Bw.
Bernhadt alipendekeza serikali kuweka njia rahisi za kuwafanya wananchi walio
wengi kuanza kufanya biashara kama kuweka njia fupi za kupata leseni na kupata
bidhaa kwa urahisi zaidi ili kushawishi mazingira rafiki kwa biashara.
Aidha
kushawishi nchi jirani kama Rwanda, Burundi na Uganda kuwekeza katika masuala
ya usafirishaji kama kuanzisha safari za ndege kutokea Bukoba kwenda Entebe, Kigali
na Bujumbura kwasababu mkoa wa Kagera ni kitovu cha nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Bw.
Bernhadt alimalizia kwa kuwakumbusha wataalam wa mkoa wa Kagera kuwa ili kutoa
huduma nzuri kwa Jamii siyo lazima uwe na mtaji mkubwa sana wa fedha mfano
huduma ya afya, alishauri kwa wananchi wenye tatizo la kutembea muda mrefu
kutafuta huduma wanaweza kujengewa vituo
vidogo vya kupatiwa huduma ya kwanza kabla ya kufika katika vituo vikubwa vya kutolea huduma za afya.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014
No comments:
Post a Comment