Umeibuka mlipuko mkubwa wa ugojwa wa Malaria, wilayani
Muleba mkoani Kagera, nchini Tanzania
ambapo tangu uibuke takribani kwa siku 11 zilizopita watoto zaidi ya 23 walio
na umri chini ya miaka 5 wameishapoteza maisha hadi juni 1, mwaka huu.
Kwa mjibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba
hadi jana jioni zaidi ya wagonjwa 203 walikuwa wamelazwa katika hospitali teule
ya Rubya iliyoko wilayani Muleba.
Vyanzo vya habari vinadai kuwa kwa sasa wagonjwa katika
hospitali hiyo wamefurika hali inayoulazimu uongozi wa hospitali hiyo kulaza
wagojwa zaidi ya wawili katika kitanda kimoja.
Hata hivyo inadaiwa kuwa vifo vilivyotokana na mlipuko kuwa vilichangiwa na hatua ya uongozi
wa halmashauri ya wilaya hiyo ya kutochukua hatua za haraka za kusambaza madawa ya kutibu huo.
Inadaiwa mapema uongozi
wa halmashauri ya wilaya ya Muleba unadaiwa ulianza kupuuzia hali ya mlipuko wa
ugonjwa huo ulishtuka baada ya vifo kuongezeka kila siku na baada ya wananchi
walipoanza kuwapigia kelele za kuomba msaada.
Maeneo yaliyokubwa na mlipuko wa ugonjwa huo ni pamoja na
yale yanayozunguka mto ngono unaoambaa hadi maeneo ya wilayani Missenyi.
Kwa hali hiyo wilaya ya Muleba wanahitaji msaada wa haraka
toka serikalini.
No comments:
Post a Comment