Tuesday, June 11, 2013

BALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI DR. KAMALA AENDELEA KUINADI TANZANIA

Mwenyekiti wa Mabalozi wa Afrika  Ubelgigiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akihitimisha  Kikao cha Mabalozi wa Afrika Ubelgiji. Balozi Kamala amewaalika Mabalozi wa Afrika na Wadau wengine wa maendeleo kuhudhuruia Mkutano wa Ushirikiano kwa Manufaa wa Wote utakaofanyika Tanzania kuanzia tarehe 28/06/2013 hadi tarehe 1/07/2013. Aidha, alizitaka nchi za Afrika na Ulaya kuimarisha Ushirikiano katika sekta ya teknolojia.
Balozi wa Tanzania ubelgiji, Uholanzi, Luxembourg , Jumuiya ya Ulaya na Taasisi ya Atomic ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akiwa na Ujumbe wa Zanzibar Uliotembelea Uholanzi . Ujumbe wa Zanzibar uliongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi mwenye koto jeupe.

No comments:

Post a Comment